KAMA ULIKUWA HUMJUI JOHARI --SOMA HAPA
Blandina Changula (amezaliwa tar. 27 Julai, 1983 mkoani Shinyanga, Tanzania.
Ni muigizaji wa vipindi vya telesheni na filamu nchini Tanzania.
Maisha ya Mwanzo
Blandina alipata elimu ya msingi
katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya
sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili
alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga
mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu
akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa
maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia
kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.
Blandina Changula anatokea kundi
la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania
kwa kutoa nyota wengi wa uigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota
hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi ( Mr Ray ), Tea na
wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group
0 comments: