WASANII KUJITOA KUSHIRIKI TUZO ZA KILI

                  IKIWA NI WIKI HII TU TANGU  MAJINA YA WASHIRIKI WATAKAOCHUANA KATIKA KINYANG"ANYIRO CHA KUWANIA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS YAMETANGAZWA,BAADHI YA WASANII HAO WAMETANGAZA KUTOSHIRIKI.

                  KILA MMOJA KWA UPANDE WAKE  WAMEDAI KUWA MASHINDANO HAYO HAYANA FAIDA YEYOTE KWAO NA WALA HAWATAPATA HASARA YOYOTE WASIPOSHIRIKI.

                 BAADHI YA WASANII HAO NI PAMOJA NA JAFARAI AMBAYE AMEANDIKA HIVI KATIKA WALL YAKE KATIKA MTANDAO WA KIJAMII WA FACEBOOK "Nimeamua kujitoa katika tuzo za mbeleni za kili music awards baada ya kugundua kama hazina umuhimu wala faida yeyote kwangu..

              NAYE MSANII DULLY SYKES AMEWAHI KUSIKIKA AKISEMA KUWA ANASHANGAA MWAKA HUU AMETAJWA TENA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYO NA WAKATI ALISHAKATAA SIKU NYINGI KUWA HATOSHIRIKI TENA
    "Nimesema na nilishasema sitaki kuwekwa katika category yoyote ile ya KIli Music Award, sioni faida ya tuzo hizo, sijawahi kupata tuzo tangu nianze mziki, single 36 mpaka sasa kama Salome,Hunifahamu na nyinginezo kibao zilizobamba lakini cha ajabu hakuna hata moja nimepata tuzo.....ni bora nitoe single tu na wala hata album sitaki.".DULLY AMBAYE ANATESA NA WIMBO WAKE WA BIBELON AMESEMA HAYUPO TAYARI KUSHIRIKI TENA MASHINDANO HAYO AMBAYO YANAFANYIKA KILA MWAKA NCHINI TANZANIA.


MPENZI MSOMAJI JE UNA MAWAZO GANI KUHUSIANA NA HALI HII?JE KUNA UKWELI WOWOTE KWAMBA WASANII HAWANUFAIKI NA TUZO HIZO? CHANGIA HAPA

Comments