MR BLUE AWACHARUKIA WANAOMUHARIBIA JINA LAKE FACEBOOK
Msanii toka katika kundi la micharazo Mr blue amewacharukia wale ambao yeye amewaita matapeli wanaotumia jina lake facebook kuwatapeli watu alafu mwisho wa siku lawama zote zinamfikia yeye (wa ukweli)
"Unajua kuna watu wananiharibia facebook,wanajiita michalazo alafu wanatapeli watu,so nikiwakamata hao nawapeleka tu polisi.kwa mfano kuna mtu anaitwa Blue Elias Byser na wengine wengi tu wanaomba show kwa raia wanatumiwa fedha kwa ajili ya show (advance),mwisho wa siku jamaa wakipata namba yangu wananiona mimi mhuni." alisema Mr Blue
Mpaka sasa Mr blue ameshawafungulia kesi raia wa Kenya ambao nao walitumia ujanja huo huo
0 comments:

