CHEKA TENA HAPA!!! KAMA MBAVU UNAZO




<b>Tatizo ni pale unapoamka asubuhi uwahi kuondoka kabla mwenye nyumba hajaamka kukuulizia deni lake halafu unamkuta kasimama mlangoni anakungoja. #HiiMaishaHii</b>
.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Tatizo ni pale umezama na binti kwenye restaurant na baada ya kumaliza kukandamiza misosi unagundua kwamba umeibiwa waleti! Yeuwooo!
,////////////.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
<b>Tatizo ni pale unapokuwa umepanda bodaboda halafu dereva wa bodaboda anakandamiza Fesibuku huku anaendesha.
</b>
<b>
Tatizo ni pale:
- Unapoenda kwenye intavyiu ya kazi unakuta boss ni jamaa ambaye mlishawahi kugombana mahali flani.
- Unapoandika status Facebook "Asante Mungu mshahara umetoka" halafu mwenye nyumba wako ana-Like.
,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.,.
- Nzi katua kwenye kipara cha mzee wako halafu unataka kumpiga kwa mkono.
- Uko kwenye daladala halafu unatupa noti ya shilingi mia 5 dirishani badala ya vocha uliyomalizia kuiweka kwenye simu.
- Baba yako anafanya kazi Tanesco halafu mmekaa home umeme unakatika unasema "Mungu na awalaani Tanesco"</b>
.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Jamaa flani kapanda daladala ana watoto wadogo wadogo kama sita hivi. Mdada mmoja pembeni yake akawa anamshangaa ikabidi amuulize: Kaka samahani, hivi hawa wote ni watoto wako? Jamaa akamcheki kwa upole halafu akamjibu: Hapana, nafanya kazi kiwanda cha kutengeneza tatu bomba, hawa watoto ni malalamiko toka kwa wateja.

.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Jamaa kakamatwa kwa kosa la wizi wa mamilioni ya vijisenti akahukumiwa kwenda jela akafungwa. Baada ya miezi miwili baba yake akamuandikia barua kwenda gerezani, jamaa akaipokea: "Mpendwa mwanangu, hali yangu ya uzee unaijua, moyo unaniuma na natamani ungekuwa hapa msimu huu wa kupanda unisaidie kulima lile shamba kule bondeni kwa ajili ya kupanda viazi, lakini sina jinsi, nafsi itaendelea kuuma na nitakusubiri mpaka mwaka utakapoaachiwa huru." Gerezani kawaida barua huwa zinasomwa kwanza na polisi magereza. Siku iliyofuata jamaa akaandika barua kumjibu baba yake: "Baba tafadhali sana wala usijaribu kulima hilo shamba la kule bondeni, pale ndipo nilipoyahifadhi yale mamilioni niliyoiba, tutaonana Mungu akipenda." Siku iliyofuata mzee akashtukia askari kibao wamevamia shamba na kulilima kila kona lakini hawakupata kitu. Baadaye jamaa akamuandikia baba yake barua tena: "Mpendwa baba, huo ndo ulikuwa msaada ambao ningeweza kufanya, unaweza kupanda viazi sasa, kwaheri."
,...........................................................................................................
Wasukuma watatu walitoka kijijini wakaenda kwa ndugu yao mjini, walipofika ndugu yao akawapa soda. Yule mmoja akaweka kizibo mfukoni, wenzake wakavitupa akashangaa! Akamnong'oneza mwenzake akasema: Wewe huchukui mbegu ya hivi vitu vitamu tukapande?
,.........................................................................................................
Jamaa yuko home kwake anaangalia mpira, mke wake akamfuata sebuleni: Mume wangu hiyo taa hapo mlangoni haiwaki vizuri, itengeneze basi. Jamaa akajibu: Nitengeneza taa wakati naangalia mpira? Hivi unaniona nafanana na mafundi umeme? Mke akanyamaza. Baada ya dakika chache akamfuata tena: Mume wangu hivi umeona meza imevunjika mguu mmoja kule jikoni? Jaribu basi kuitengeneza. Jamaa akamcheki halafu akajibu: Hivi we mwanamke una nini? Ukiniangalia nafanana na mafundi seremala? Mke akaguna halafu akaondoka. Baada ya muda akarudi tena: Baba watoto, hapo kwenye ngazi mlangoni umeona tofali moja limetoka? Jaribu basi kulirudishia. Jamaa kwa hasira akajibu: Hivi hupendi kuona mtu amekaa kwa starehe? Mimi nafanana na mafundi ujenzi?

.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Baada ya kuona anasumbuliwa jamaa akaamua aende zake kuangalia mpira baa. Akiwa anacheki mpira nafsi ikamsuta kwamba alichomfanyia mkewe si kizuri akaamua kurudi home kumuomba msamaha. Alipofika akukuta tofali mlangoni limetengenezwa, meza jikoni nayo imetengenezwa na hata taa mlangoni nayo imeshatengenezwa, akashangaa akamuuliza mkewe vipi? Mkewe akajibu: Alikuja Kiwango Dungadunga yule kaka wa nyumba ya jirani akanisaidia ila kwa masharti kwamba, nimtengenezee ice cream au nikalale kwake lisaa limoja. Jamaa akajibu: Dungadunga mjinga kweli, kwa hiyo ukamtengenezea hiyo ice cream. Mke ajibu: Kwani mimi nafanana na kiwanda cha bakhresa?
.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,