USIPATE TAABU..UKIMFANYIA MAMBO HAYA MPENZI WAKO HAWEZI KUKUACHA KIZEMBE

 
1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.

2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.

3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali

4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.

5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.

6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini

7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.

8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.

9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.

10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia




NJIA YA KUMFANYA MSICHANA WAKO AKUPENDE DAIMA

.


1. Ipende familia yake(wazazi, kaka au dada zake) kwa ukaribu. Jaribu kuwaandalia zawadi katika sikuku mbalimbali na kuwaonesha kuwajali. Itamfanya aone unamjali yeye pamoja na familia yake.

2 akiwa katika hali ambayo si nzuri yaani hana raha au kuuziwa na mtu mwingine mtazame machoni ukiwa unatabasamu na umsifie yeye ni msichana mzuri kuliko yeyote aliyewahi kuzaliwa katika hii dunia kisha mkumbatie.

3. Anapoanza kulia usithubutu kuzungumza chochote. Mkumbatie na kuzichezea nywele zake kwa kuzipapasa akiwa kifuani mwako. Hujihisi faraja na kujiona yupo

mahala salama kuliko yeyote

4 jitahidi kumpikia chakula akipendacho siku akikutembelea nyumbani kwako ama geto na ukipatie sawa sawa hii itamfanya kukuona wewe ni mvulana unayefaa kuwa mume wake.

5 usizungumze naye sana kuhusu mambo ya kufanya mapenzi, hii itamfanya kukuogopa atahisi una nia ya kumchezea kisha umuache. Kwa mwanamke ambaye upo naye serious hakikisha uligusii sana hili katika uwepo wenu tulivu chumbani labda mara chache mkizidiwa hii itamfanya aone wewe ni mwanaume usiye na tamaa ya ngono.

6 jitahidi kujua vitu ambavyo anapendelea. Mfanyie mara kwa mara vitu hivyo itamfanya kutamani kuwa na wewe muda wote na kukukumbuka pale anapokuwa mbali na wewe.

7 jitahidi kumuuliza mara kwa mara kuhusu siku yake imeendaje kama atakuwa ameboreka na mtu aliyemuuzi mbembeleze kwa kumfariji asiwe na hasira itamfanya kukuambia kila linalomuuzi akiamini furaha pekee ipo kwako.

8 mwanamke hapendi ugomvi kelele na kupigwapigwa hata kama amekuuzi usimkaripie ni heri kama kuna kitu umesikia kaa dakika chache mpaka hasira zipungue kisha ndio umuulize kwa upole atakuona ni mwanaume mwenye busara hivyo hata kama itakuwa ni kweli basi atakueleza ukweli bila kukuficha hii utokana na moyo utamsuta kwa kile alichokifanya ukiwa mpole kwake.


9 kuwa muongeaji sana mwenye hadithi mbalimbali za kuvutia unapokuwa naye. Itamfanya asiatamani kukaa mbali nawe. Sio unakaa kisha unataka yeye ndiye azungumze ataaga mapema na kuona bored utakapokuwa unamuita mara nyingine ataona unamchosha huna story huna jipya.

10. Kuwa mwenye mipango endelevu. Hakikisha ubweteki na kuridhika na hapo ulipo hakikisha unamueleza msichana wako kila unachozani kizuri katika kuwakwamua katika hatua fulani kwenda nyingine itamfanya aone wewe utakuwa baba bora baadaye

0 comments: