Kwa muda wa miezi mitatu msanii nyota wa bongo flava Diamond Platnium ameonekana kuelemewa na mzigo wa skendo ambazo zina lengo la kumharibia jina au kumshusha kabisa heshima yake aliyoiweka kwa mashabiki wake...
Msanii huyo kama una kumbuka aliwahi kupata skendo ya kukopi idea ya wimbo wa Nataka kulewa ya kwake H baba na kuirekodi yeye wakati H baba akiwa hana taarifa.Baadae hbaba baada ya kuisikia wimbo wa Diamond mtaani akaenda katika vyombo vya habari kulalamika.
Kama hiyo haitoshi msanii huyo pia amewahi kupata balaa nyingine pale katika ukumbi wa maisha clab alipokuwa anapiga show,lakini amani ikavurugika ukumbini humo kwa sabau ya vurugu zilizoanzishwa na watu wasiofahamika.na kumletea Hasarakubwa ikiwemo kupoteza kwa kamera yake ya matukio.
KUBWA ZAIDI ambalo kwa sasa linaongelewa sana mitaani ni hii ya UCHAWI,Ambapo mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mganga wa diamond kuibuka katika vyombo vya habari na kulalamika kwamba Tangu amemtengeneza Diamond aweze kukubalik kwa watu msaniii huyo amekuwa akimgeuka na hataki kabisa kukutana na mganga huyo tena,Na mganga huyo kutangaza kuwa atafnya mambo yake tena ili kumshusha msanii huyo..
Kutokana na matukio yote haya,msanii huyo ameonekana kuwa ndio msanii mwenye skendo kubwa kwa mwaka huu tangu uanze....