LULU HUYOOOO MTAANI

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam. Lulu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, ambaye hata hivyo baadaye alibadilishiwa kesi na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia. Msanii huyo ameachiwa huku akipewa masharti ya kuacha Hati ya Kusafiria Mahakamani, kuripoti Mahakamani kila tarehe mosi, pamoja na wadhamini wawili waliotoa milioni 20 mmoja. Kwa wiki kadhaa sasa, baadhi ya watu wamekuwa wakisikika wakiomba dua njema kwa msanii huyo ili aweze kuachiwa kwa dhamana na kufuatilia kesi yake akiwa nje na familia yake.

0 comments:

Post a Comment

sema nasi hapa!!