HIKI NDICHO KILICHOJIRI EATV AWARDS 2016 MPAKA KUFIKA LEO HII

TUZO za EATV zimeanzishwa mwaka 2016 na kampuni ya East Africa Television na Radio, zitafanyika kwa mara ya kwanza tarehe 10/12/2016 jijini Dar Es Salaam,Tanzania.

Tuzo hizi zinashirikisha wasanii wa muziki na filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na zitakuwa zikifanyika kila mwaka, huku vipengele vya tuzo vikiongezeka kila mwaka kutoka vipengele kumi vinavyoshindaniwa mwaka huu.

Kuanzishwa kwa tuzo hizi kuna lengo la kuthamini wasanii na kuleta ushindani kwenye sekta hii ya sanaa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Dominican Mkama, Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar es Salaam kutoka Vodacom amewataja wasanii watano wanaowania kipengele cha 'Muigizaji Bora wa Kiume' na wanamuziki watano wanaowania kipengele cha "Mwanamuziki Bora Chipukizi"
MUIGIZAJI BORA  WA KIUME
Nominee: Saidi Ally filamu aliyoigiza (Ndugu wa mume)
Nominee: Meya Shabani Hamisi filamu aliyoigiza (Facebook profile)
Nominee: Salim Ahmed (Gabo) filamu aliyoigiza (Safari ya Gwalu)
Nominee: Dotto Husein Matotola filamu aliyoigiza (Likwacha lala)
Nominee: Daudi Michael Tairo filamu aliyoigiza (Mfadhili wangu)
MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Nominee: Amani Hamisi (Man Fongo); Wimbo - Haina Ushemeji
Nominee: Feza Kessy; Wimbo - Sanuka
Nominee: Rukia Jumbe (Rucky baby) ; Wimbo - Give Me Some More
Nominee: Mayunga Nalimi (Mayunga) ; Wimbo - Nice Couple
Nominee: Rashid Said (Bright) ; Wimbo - Nitunze

KUWAJUA NOMINEES WOTE BOFYA HAPA