WIMBO MPYA MTEMI PESA BY SQUEEZER


BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva, George Kassela ‘Squeezer’ ameibuka na kusambaza kazi yake mpya ya ‘Mtemi Pesa’. Katika wimbo huo mkali huyo amemshirikisha msanii wa bongo fleva, ambaye pia anafanya vizuri katika tasnia hiyo, Abednego Damian ‘Belle 9’.