SOMA HABARI YA KUHUSU TRACK YA KIBIBI YA ABDU KIBA


MKALI wa bongo fleva nchini, Abdukarim Kiba ‘Abdukiba’ anatarajia kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kibibi’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Abdukiba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi zake, ambapo anatarajia kuisambaza mwishoni mwa wiki hii.
“Sipendi kuzungumzia ndani yake kuna nini, naomba mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea kazi hii, kutokana na ujumbe uliomo ndani yake,” alisema.
Alisema wapenzi wa kazi zake wamsubiri sokoni ana imani kazi hiyo itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliomo ndani yake, licha ya kukaa kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kutoa kazi mpya.