MWAKA 2013 NDIO UNAELEKEA MWISHONI KABLA YA KUINGIA MWAKA 2014 KAMA MUNGU AKITUJALIA UHAI,KWANI UMEBAKI MWEZI NA NA SIKU CHACHE TU KABALA HATUJAUACHA MWAKA HUU...LAKINI PIA MWAKA HUU UMEKUWA NI MWAKA WA MAJONZI KWA WAPENDA SANAA HAPA NCHINI KWETU KWANI TUMEWAPOTEZA WASANII WETU WENGI TUWAPENDAO KWA NYAKATI TOFAUTI TOFAUTI NA SABABU TOFAUTI TOFAUTI.MIONGONI MWA WASANII HAO NI KAMA IFUATAVYO HAPA CHINI IKIWA PAMOJA NA PICHA ZAO
02/01/2013
Msanii aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu,Sadick Juma Kilowoko ama aliyetambulika sana katika tasnia ya Filamu hapa nchini kwa jina la kisanii Sajuki,alifariki Dunia MUNGU AKUPUMZISHE PEMA
08-01-2013
MSANII maarufu wa Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu
28-05-2013
msanii maarufu wa Hip Hop nchini,Albert Mangwair (Mangwea) alifariki dunia nchini Afrika Kusini katika hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johanesburg alipopelekwa baada ya kugunduliwa na wenzake asubuhi kwamba alikuwa hoi. Hali hiyo ilimkuta maeneo ya Brixton-Mayfair West ambapo alikuwa amefikia kwa rafiki yake ambaye walisoma wote miaka ya nyuma.
13-07-2013
Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) alifariki dunia.
10-07-2013
Kash (Jaji Khadija) amefariki dunia katika hopsital ya muhimbili ambapo alikua amelazwa. Kash amewahi kutamba sana katika Michezo ya kuigiza kipindi cha nyuma kidogo iliyokua ikirushwa ITV, hadi mauti yana mkuta amekua akijuhusisha na shughuli za kuigiza. Moja ya Igizo alilowahi kucheza ni Tamu Chungu
17-04-2013
Aliyekuwa nguli wa muziki wa mwambao Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Bi Kidude alifariki tarehe hiyo
September 08, 2013
Mwigizaji Zuhura Maftah Maarufu Kama Melissa Afariki Dunia .Kwa taarifa tulizozipata ni kwamba Zuhura aliumwa week chache Ni mwigizaji aliyefanya kazi na bongo movie kwa ukaribu kabla ya kutoka na kuanza kufanya kazi zake binafsi
Msanii wa taarab nchini anayejulikana kwa jina la Nyawana Fundikira aliyetamba na wimbo wa 'Nipo Kamili Nimejipanga', pia alifariki mwaka huu 2013
pia kwa mwaka 2012 vifo vya wasanii kama sharo milionea,john maganga,steven kanumba,mariamu khamisi na wengine haviwezi kusahaulika.mungu awalaze wasanii wetu tuliowapenda mahali pema peponi
sharo milionea → November 26, 2012 |
steven kanumba April 7, 2012 |
Mungu awalaze wasanii wetu tuliowapenda mahali pema peponi