BAADA ya kufanya vizuri na kazi yake ya ‘Salamu Zao’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibarik ‘Ney wa Mitego’, anajipanga kusambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Nakula Ujana’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ney alisema wimbo huo ameutoa maalumu kwa wale wote ambao wanasema yeye anabahatisha katika nyimbo zake, hivyo kuna ujumbe wa kutosha ndani yake.
“Wengi wameongea sana kuhusu baadhi ya nyimbo zangu, mimi nataka kuwaambia kama mimi sibahatishi niko kikazi zaidi; ‘Muziki Gani’ wanasema Diamond ndiye kanisaidia, sijui katika ‘Salamu Zao’ nani kanisaidia!