HAINA JINA BY SOGGY DOGGY OFFICIAL VIDEO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Anslem Tryphone ‘Soggy Doggy’ amesambaza video ya kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Haina Jina’ ambayo amemshirikisha chipukizi wa muziki huo, Abbas Kubaff. Soggy alishawahi kutamba na kazi zake nyingi ikiwamo ‘Kibanda cha Simu’ ambayo ilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na maudhui yaliyomo ndani yake.