NAJA NA VIDEO YA MILLION 15-BOB JUNIOR

MUIMBAJI na mtayarishaji wa muziki nchini, Raheem Ramadhan ‘Bob Junior’, ametenga dola 10,000 za Marekani, takriban sh milioni 15, kwa ajili ya kukamilisha video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Bahasha’. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Bob Junior alisema kuwa wimbo huo amemshirikisha msanii anayekuja juu kwa kasi hivi sasa, Vanessa Mdee, na video hiyo itafanywa na kampuni ya Ogopa Videos ya Kenya. Bob Junior alisema kuwa wimbo huo umepokelewa vizuri na mashabiki kuliko ngoma zote alizowahi kufanya toka kuanza kwake muziki.