vunja mbavu na huyu mlevi

Mlevi mmoja alikuwa anapita kando ya mto, mara akamwona Pastor anawabatiza watu. Akaamua na yeye kujiunga kwenye foleni, ilipofika zamu yake akazamishwa mara ya kwanza. Akaulizwa ''umempokea YESU? Akajibu ''hapana'' akazamishwa tena, akaulizwa ''umempokea YESU? Akasema ''hapana'' akazamishwa mara ya tatu, akaulizwa ''umempokea YESU? Akajibu ''HIVI UNA UHAKIKA ALIZAMA HAPA? Au unanisumbua tu.


Katika safari kulikuwa na MZUNGU, MCHINA ,MMASAI & MCHAGA, ...
Wakiwa katikati ya safari meli ikaanza dhoruba na kuelekea kutaka kuzama, ikalazimika kila mtu atupe baharini mizigo aliyobeba,
akaanza MZUNGU akatupa computer hukuakisema "TUTATENGENEZA ZINGINE ULAYA".
Akafuatia MCHINA akatupa mabox ya simu huku akisema "ZIPO NYINGI CHINA" akafuatia MMASAI akatupa ng'ombe huku akisema "ZITAZALIANA ZINGINE" akafuatia MCHAGA ,kila kitu alichobeba anakiona kinathamani, akaamua kumtupa mmasai huku akisema "WAPO WENGI KULE KWETU MONDULI!"


Mtoto katoka shuleni huku analia, alipofika nyumbani. Baba yake akamuuliza ''unalia nini'? MTOTO '' Nimepigwa na mwalimu na nimeambiwa twende wote shuleni''. Wakaenda shuleni na wakaingia ofisini. MWALIMU ''Karibuni, mtoto wako tumemuuliza Nairobi iko wapi kashindwa, ndio maana tumemchapa'' Baba akamgeukia mtoto wake na kumpiga vibao, akamwambia ''mpumbavu mkubwa, kila siku nakukataza kuchezea vitu vya watu hukomi, haya NAIROBI ya mwalimu umepeleka wapi'?

Comments