Katika hatua ambayo imeshtua na kukasirisha wengi, mahakama ya rufaa California imepindua kesi ya ubakaji kwa kusema ilikuwa siyo ubakaji kwa sababu "mhasiriwa alikuwa hajaolewa".
Morales Julio Alikamatwa kwa madai ya ubakaji mwaka 2009 baada ya kudaiwa kumdhalilishwa kingono mwanamke wa 18.Mwanamke huyo aliiambia mahakama , yeye na mpenzi wake walikuwa ni wapenzi lakini waliweka ahadi ya kutofanya mapenzi mpaka wakifunga ndoa.anasema siku moja akiwa amelala alihisi mtu akimbusu shavuni lakini alitulia akijua ni mpenzi wake na hiyo ilikuwa ni kawaida yao kubusiana. Anadai kuwa kwa kuwa alishazima taa hakuwa na wasiwasi lakini kumbe hakuwa ni mpenzi wake bali ni lrafiki wampenzi wake.Baadae mwanaume huyo alianza kufanya mapenzi na baada ya kugundua kuwa sio mpenzi wake alimwomba amuachie lakini mwanaume(morales) huyo aliendelea mpaka alipomaliza.
Morales alishtakiwa kwa ubakaji na wakati kesi yake akaenda mahakamani,Majaji waliiambia wahudhuriaji hawakuweza kumpatia hatia ya ubakaji kwa kuwa kwanza alikuwa amelala na pili kwa kuwa alikuwa hajaolewa bado. Hata hivyo, chini ya sheria ya sasa California, ubakaji na udanganyifu au impersonation husika tu kama mwanamke ameolewa.
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!