Msiba mwingine ndani ya Bongo movie @Sajuki afariki DUNIA,KUZIKWA KISUTU

sajuki kabla hajaanza kuumwa
bibi wa sajuki akiwasili msibani
mwigizaji mahiri Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Sajuki aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba 2012, alikofikishwa akitokea Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya kuanguka jukwaani jijini Arusha, alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake ikiwa ni harakati za kutafuta fedha michango ya pesa za kumpeleka tena India kupata matibabu.




sajuki akisaidiwa kutembea baada ya kuanguka stejini
sajuki baada ya kuanza kuumwa
`Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India.
Makubi alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na msanii huyo kwa ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya mazishio yake.
Kabla na baada ya kuifika India kwa matibabu, Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini, ambapo aliporejea alionekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
        
Kifo cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii nguli wa filamu na muziki ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven Kanumba, John Maganga, Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ walifariki kwa nyakati tofauti kutokana na maradhi na ajali.

SAJUKI ATAZIKWA IJUMAA KATIKA MAKABULI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

Comments