Terry Connor sasa meneja wa Wolves

Klabu ya Wolves imempandisha cheo meneja msaidizi wa Wolves.
Terry Connor sasa atashikilia madaraka hayo ya meneja hadi mwisho wa msimu.
Klabu kilimfuta kazi Mick McCarthy tarehe 13 Februari mara tu baada ya kushindwa magoli 5-1 na mahasimu wao West Brom.
Wolves wameamua kumpandisha cheo Connor baada ya Walter Smith, Alan Curbishley na Brain McDermott kuamua hawaitaki kazi hiyo ya kuiongoza Wolves.
"Hii ni hatua muwafaka ambayo ina msimamo halisi. Wachezaji wanaiunga mkono kikamilifu", ameelezea tajiri anayemiliki klabu ya Wolves, Steve Morgan.
"Tangu tulipofanya uamuzi kwa shida kuachana na Mick, tumepitia utaratibu kwa makini katika kumchagua mtu atakayefaa.
"Baada ya kushauriana na watu kadha katika utaratibu huu, mimi na bodi tumeamua kwa pamoja Terry ndiye mtu atakayefaa kukiongoza klabu hadi mwisho wa msimu".

kutoka bbc swahili

Comments