TAIFA STARS VS DRC 23 FEB

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF kupitia kwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura; mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo viti  vya kijani na bluu vinachukua watazamaji 36,693 ambayo ni karibu theluthi mbili ya viti vyote kwenye uwanja huo wa kisasa na kiingilio kitakuwa ni tsh 2000/- kwa viti hivyo.
DRC  
Amesema viti vya rangi ya chungwa kiingilio ni sh. 5,000, VIP C itakuwa sh. 7,000 wakati VIP B tiketi zitauzwa kwa sh. 10,000. Kiingilio kwa viti vya VIP A kitakuwa sh. 15,000. Kwa vile Februari 23 mwaka huu ni siku ya kazi ili kutoa fursa kwa washabiki wengi kushuhudia pambano hilo la kimataifa, mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni.
            

TAIFA STARS         
 

Comments