POLISI WANNE MATATANI SONGEA



Kufuatia fujo zilizozuka wiki hii mjini songea kati ya polisi na raia waliokuwa wanawataka polisi kufuatilia na kuwatia mbaroni watu waliokuwa wanafanya mauaji mjini hapo,na kusababisha raia wawili kuuwawa kwa risasi.Jeshi la polisi limewatia hatiani polisi wanne ili kujibu na kuelezea sababu zilizo wafanya kutumia risasi kwa raia..Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda alisema jana kuwa askari hao walikamatwa na wanaendelea kuhojiwa ili kujua kama kulikuwa na uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao.“Kwa kuwa tukio hilo limehusisha vifo, hatuwezi kuacha hivihivi tu ni lazima tujiridhishe kuwa askari hao hawakufyatua risasi kwa uzembe,”alisema Kamhanda. Kamanda huyo alisema askari hao watahojiwa baada ya kuundwa kwa tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo, na tume hiyo ikibaini kuwa kulikuwa na uzembe, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwamo kufikishwa mahakamani.
Juzi wananchi waliokuwa wakiandama kupinga mauaji hayo, walipambana na polisi ambapo watu wanne waliuawa na wengine 41  kujeruhiwa.

Hali za majeruhi  Majeruhi wanane kati ya 11 waliolazwa katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma, jana waliruhusiwa. Majeruhi wengine 30 walipatiwa matibabu juzi na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwao.

 Mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Benedicto Ngaiza alisema tayari wagonjwa  wanane kati ya kumi na moja waliolazwa katika hospitali hiyo wameruhusiwa na kwamba ni wagonjwa watutu ndio waliobaki.
 kwa mara nyingine, jana saa 12 jioni,  polisi mjini Songea walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwaokoa watu wawili waliokuwa wakipigwa na wananchi wakiwatuhumu kwamba ni majambazi wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya wananchi.Watu hao ambao walijeruhiwa vibaya walikamatwa na wananchi katika eneo la Mkuzo nje kidogo ya Manispaa ya Songea baada ya kujitambulisha kwa wenyeji kwamba wao walikuwa wakitatafuta shamba la kununua, huku mmoja wao ambaye ni mwanamke akitoroka na kukimbilia kusikojulikana.

Kutokana na kuwatilia mashaka, wananchi hao waliwazingira na kuwaweka chini ya ulinzi kisha kuwafikisha nyumbani kwa kiongozi wa Serikali ya mtaa wa Mkuzo, John Moyo na baadaye walianza kuwapiga baada ya kutokea utata katika maelezo yao.

Kuona hivyo moyo alipiga simu polisi ambao walifika na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi, hivyo kuwaokoa watuhumiwa hao kisha kuwakimbiza katika hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu.

Watuhumiwa hao ambao wametambuliwa kwa majina ya Gervase na Juma, walikuwa wakivuja damu katika sehemu kadhaa za miili yao na polisi walipowafanyia upekuzi waliwakuta wakiwa na hirizi na nyaraka zilizoandikwa kwa lugha ambayo haikuwa rahisi kusomeka.

Comments