Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina lake jana mchana {IJUMAA} alitoroka na gari ya zima moto akiwa mtupu kabisa katika mji wa South Carolina, na kumuua mtu mmoja aliyekuwa anapita barabarani
Polisi wamesema mtu huyo ambaye hakuwa na kitambulisho kama ni mfanya kazi wa kampuni hiyo ya uokoaji alirukia gari hilo na kondoka nalo kwa spidi kali mara baada ya kusikia simu ya hatari iliyokuwa ndani ya gari.Baada ya kumfukuzia kwa muda mtu huyo alitolewa nje ya gari mara baada ya kugongesha gari hilo katika mti mmoja na kusababisha uharibifu wa mali hiyo.lakini cha ajabu alianza kupigana na polisi hao na waokoaji waliokuwa wanamfukuzia kumuokoa .
Shuhuda wa ajali hiyo anasema hivi "sikuwahi kuona gari ya moto inakimbia hivo hata siku moja," Rogerson alisema . "halikuwa limewasha taa wala king'ola"
Haijafahamika kam mtu huyo alikuwa na ugonjwa wa akili au la.Polisi wamemtaja mtu aliyegongwa na gari hilo kuwa ni Justin Miller mwenye miaka 28 kutoka Port Royal pia gari hilo liliharibu magari kadhaa yaliyokuwa katika barabara lililopita gari hilo la zima moto.DUNIANI KWELI KUNA VIOJA
Hiyo ndo state kaka, kila kukicha mtu anafanya kioja ili awe maarufu. Am not suprised.
ReplyDeletedah ila huyo ni mkali dah!!
Delete