• Studio iliyotolewa na Mh Rais kurudishwa na kukabidhiwa Chama halali cha kutetea wasanii(TUMA) kinachotambuliwa na BASATA .
• Chama feki cha wasanii TFU kuvunjwa na wasanii kuambiwa kujisajili na chama cha TUMA kwa utaratibu uliopo.(hakuna ubaguzi)
• Maboresho ya malipo kwa wasanii katika maonyesho.
• Kuachwa mara moja kwa mizengwe iliyokuwa inafanywa na redio yao ya kutopiga nyimbo za wasanii mbalimbali kwa kigezo cha chuki na rushwa.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyokubaliwa kutekelezwa na hatuoni kwanini tuendelee kukataa wito wa kumaliza suala hili na iwapo kama hawatatekeleza kama walivyosema hapo jamii itatuelewa kuwa sie sio wakorofi na tulikuwa na dhamira ya dhati katika kupata suluhisho la suala hili.
Tunathamini juhudi zote za upatanishi wa suala hili uliofanywa na waheshimiwa wote katika hili ilikuleta tija na maelewano ya kweli tunataka haya yazingatiwe ili kutekeleza muafaka huu na kutimiza dhana ya dhati ya kusaidia sanaa yetu na wasanii wetu kwa ujumla wake.
Tunaomba haya yafuatayo yazingatiwe na kuwekewa mkazo:-
- Pande hizi mbili zikutanishwe tena kwa nia ya kuweka mambo sawa kwa vyombo vya habari ili kuondoa ile hali ya sintofahamu ilijitokeza na kuchanganya wanajamii nchini kuwa, makubaliano hayo yaliyofanyika ni ya watu binafsi kati ya Sugu na Ruge (waliokuwa na ugomvi kwa zaidi ya miaka 10 sasa) na kamwe hayahusishi kundi la Vinega wa anti virus na redio nzima ya Clouds fm.
- Bwana Rugemalila kutekeleza yale yote yalizungumziwa kuwa chanzo cha magomvi haya pamoja na kutoa suluhisho la tatizo la tuhuma za rushwa na upendeleo katika redio yao.Suala la mfanyakazi wao Othman Suka wa kitengo cha muziki kuwa kinara wa rushwa na upendeleo katika muziki pale redioni kwao pia lizingatiwe ili kupata muafaka wa kweli vinginevyo tatizo baso litaendelea kuwepo.
- Watangazaji wa Clouds Fm na menejimenti yao kuzingatia muafaka huu na kujiepusha na kauli zozote zitakazouweka muafaka huu katika hali ya mashaka,kauli za kejeli za Adam Mchomvu,DJ Fetty,B 12,Ncha kali na wenzake hakika zitauvunja muafaka huu na kurudisha suala hili lilipotoka.
- Utekelezaji ya yaliokubaliwa uende na wakati na katika hili dhamira ya kweli ya kutimiza haya ionekane.
- Kila upande ukaamini kuwa haya yote yamefikiwa kwa ajili ya manufaa ya wasanii wote na si kwa maslahi ya wachache ili makubaliano ya kuivunja TFU na wasanii wote kujiungana TUMA chama cha wasanii kilichosajiliwa BASATA nila kufanyika mapema ili kupata mwanzo mpya katika sanaa yetu.
- Tunaomba watanzania wenzetu waliotuunga mkono waone haya mapatanisho ni ushindi kwa vinega wote kwani tuliopigania yamekubaliwa utekelezaji pamoja na upungufu katika kutoa taarifa kwa mpangilio. Tunaomba watuunge tunavyoendelea na safari ngumu iliopo Mbele yetu.
- Miongoni mwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaondoa mfumo wote mbovu unounganisha watu wengi wakiwemo wakurugenzi/mameneja masoko wa makampuni kung’ang’ania kufanya kazi na radio moja na makampuni yake tu ili kuficha rushwa iliokithiri baina yao na kuwahimiza wapanue fursa kwa watanzania wote wenye uwezo wa kuandaa shughuli; kuhimiza redio na watumiaji wengine wa kazi za wasanii kulipa mirabaha watakayokubaliana kwa pamoja na TUMA kwa kutambua wasanii ndio chanzo cha mapato ya tasnia hii na wafanyabiashara wote katika sanaa waone ushirikiano na wasanii ndio njia ya kupata kipato kikubwa na kisicho na tafran, kuondoa woga wa wasanii kujiunga pamoja katika chombo chao ili kupata haki zao kama Vinega tulivothibitsha inawezekana na kuwasaidia wasanii watambue mchango mzuri wa redio na wafanyabiashara watakaofanya biashara nao kwa utaratibu utakaowekwa; Na kuendelea kuithibitishia Serikali na vyombo vyake vyote kama Bunge, TRA, Jeshi la Polisi, Mahakama nk ni manufaa kwao waamke na kufanya kazi ya dhati na TUMA na wadau wengine kuipanga hii “industry” ya SANAA ili kuboresha pato na maisha ya watanzania.
Pongezi zetu kwa Mh Jenista Mhagama(MB) ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii,Mh Nchimbi Waziri wa Habari na Utamaduni,Mh Tundu Lissu(MB) na wote waliosaidia kumaliza suala hili,Tunaamini kuwa kwa dhamira ya dhati tunaweza kuwakomboa vijana hawa wanaotuamini sisi na kuweka mifumo bora itakayowafanya wasanii wa nchi hii kufaidika na sanaa zao kama wenzetu wa Kenya,Uganda na kwingineko.
Tunapenda kuwapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine walighafilika na kuwa katika wakati mgumu kutokana na jambo hili,na wito wetu sisi Vinega kwa mashabiki na wanaharakati wote ni kuwa…..bado tunayo kazi kubwa ya kuendeleza haya mapambano kwa faida ya vizazi vijavyo na tusibweteke kwa ushindi huu na pia tusiupuuze ushindi huu kwani ndio njia zinafunguka kuelekea kwenye mafanikio.
HARAKATI DAIMA
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!