SUGU,RUGE SASA "KITU KIMOJA"

HIVI KARIBUNI WATANZANIA WALIOKUWA WANAFUATILIA MGOGORO KATI YA MR 2,NA RUGE WACLOUDS FM KUHUSU MALALAMIKO YA SUGU NA CREW YAKE YA ANT VIRUS KUWA RUGE AKISHIRIKIANA NA BAADHI YA WATU FLANI WANAUHUJUMU MUZIKI WA BONGO  NA WASANII WAKE,WAMEBAKI VINYWA WAZI BAADA YA 'BIFU' HILO KUMALIZIKA KIURAHISIIIIII!!! KAMA ANAVYOELEZEA MWENYEWE SUGU HAPA

“ni kweli tulikua katika vita na vita lazima ifike mwisho labda iwe ni vita isiyo na malengo ndio haitaki suluhu lakini kama ilikua na malengo ina maana inapopatikana fursa ya suluhu kama kweli ulikua na dhamira a dhati kwa kile unachokipigania lazima ukubali kukaa chini na kutafuta suluhu ili tusonge mbele, tumekubaliana, sasa tunasonga mbele na wengine sasa hivi tupate fursa sasa hivi kujikita zaidi kwenye siasa za kitaifa” ALISEMA SUGU AKA MR 2

Comments