KWA SMS HIZI BASI USIPOCHEKA BASI UTAKUWA UNA TATIZO LA KIAFYA


MAMA: He mwalimu hujambo? MWALIMU: Sijambo Mama Devi, tena bahati tumekutana ilikuwa tukutafute tuongee kuhusu Devi MAMA: Nini tena huyu mtoto? MWALIMU: Devi ana akili sana, lakini tatizo lake anapenda sana kuchokoza na kucheza na wasichana, hivyo waalimu tumeona tujaribu kutafuta dawa tumkomeshe hiyo tabia MAMA: Yaani mwalimu mkipata hiyo dawa ntaiomba nimtibu baba yake, naye yuko hivyohivyo

MDADA: Mpenzi wangu mbona huwa hutabasamu hata kidogo ukiwa na mimi? MKAKA: Jamani si we mwenyewe ulisema unataka tuwe siriaz kwenye mapenzi yetu? Nikaona nikichekacheka utaniacha

Jamaa kamuomba Mungu....Ee Mungu nijalie kazi niwe na mifuko imejaa hela kila siku, gari limejaa mademu kibao, niwe nikifungua mdomo watu wananisikiliza...wiki moja baadae jamaa akapata kazi ya ukonda kwenye daladala

DAVINA: Mambo Sandra, mwenzio nimenunua bonge ya simu
SANDRA: Simu gani? Itakuwa Mchina maana wewe unapenda vya urahisi
DAVINA: A wapi nina Blackberry
SANDRA : Hongera, Blackberry yako Samsung au Nokia
DAVINA: Unanionaje? Kitu Erricson  hiki bibie 
 Mjamaa alikwenda mji mmoja jina kapuni kumtembelea rafiki yake, chakula kikaja, akajikuta kapewa ugali na nyama nyingi na mwenyeji wake pia akapewa ugali na nyama nyingi, watoto na mke wakawa pembeni wanakula ugali na mboga za majani. Jamaa lika mtach lakini akanyamaza akapanga wakimaliza kula amuulize rafiki yake kwa nini anafanya uchoyo huu. Walipomaliza sahani zimekwisha tolewa na baada ya kunywa maji baridiiiiiii;
JAMAA: Aise sijapenda hii tabia, sisi tumekula ugali na nyama kibao mkeo na watoto wamekula mboga za majani bila hata kipande cha nyama
MWENYEJI:Mi sio kosa langu, wao wenyewe hawataki kabisa kula nyama ya mbwa

 MKAKA: Hi uwapi swity?
MDADA: Niko home
MKAKA: Unafanya nini?
MDADA: Nakula
MKAKA: Unakula nini?
MDADA: Mama katengeneza macaroni, ambayo kanyunyizia chiizi na  sausage fulani imported ambazo baba amenunua supermaketi Masaki, na saladi, kisha ntateremsha na Epo juisi, ghafla ikasikika sauti ya mama yake
MAMA: Hivi we Gulo kaka yako atakula nini na we umemaliza ugali na maharage yote?
 

0 comments: