TEMBA NAE ALIZWA VIFAA VYA GARI LAKE

gari ya j.wolper baada ya kuchomwa na watu wasiofahamika
WIMBI la wasanii kuibiwa na kuharibiwa magari sasa limeshamiri sana hapa bongo Dar es salaam,kwani ikiwa zimepita siku chahce tangu mwanadada Wolper kuchomewa moto gari lake akiwa amepaki nyumbani kwake,Sumalee nae kuibiwa gari lake maeneo ya Coco beach,Ommy dimpozi kuibiwa vifaa vya gari lake pia Alfajiri ya kuamkia leo, Mh Temba ameibiwa vifaa vya  gari lake aina ya Verossa akiwa amelipaki nyumbani kwake.Temba amesema vifaa vilivyoibiwa ni pamoja na power window, side mirror zote taa za nyuma, radio leseni,na vinginevyo ambavyo thamani yake hajaijua kwa sasa.

"jamaa siwajui ila wamekuja na wameniibia power window, taa za nyuma, sidemirror vitu vya ndani wameiba radio, leseni hadi madaftari yangu ya shule, makaratasi, sasa sijui atakua ametumwa au anafanya maksudi yaani anaiba mpaka madaftari" amesema temba

Comments