MAUAJI YA MADEREVE BODABODA YAZIDI KUSHAMIRI NCHINI


 
WATU wanaodaiwa kuwa ni vibaka wamemuua kwa kumpiga na kitu kizito katika paji la uso, dereva bodaboda, Abeli Nyunza eneo la National mjini Iringa na kumpora pikipiki yake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Muungano Frelimo mjini Iringa jirani na shule ya msingi Muungano.
Wakielezea juu ya tukio hilo, mashuhuda waliozungumza na mtandao wa http://francisgodwin.blogspot.com/ wamedai kuwa majira ya usiku walisikia mlio wa pikipiki na ghafla ulizimika na baada ya hapo ilisikika sauti ikiita kwa nguvu Peter! Peter ! mfano wa mtu aliyekuwa akiomba msaada na baada ya dakika kama 10 hivi ukimya ulitanda na ghafla ulisikika mlio wa pikipiki iliyokuwa ikiondoka kwa kasi.
Mwenyekiti wa bodaboda mjini Iringa, Macurius Chengulla mbali ya kuthibitisha kifo cha dereva bodaboda mwenzao huyo bado amesema kuwa wameweka mkakati wa kuendesha msako ili kuwabana wahusika wa mauaji hayo.
Chengulla amesema kuwa matukio hayo ya kuuawa kwa madereva bodaboda kwa manispaa ya Iringa ni tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya kutekwa na kujeruhiwa yamekuwa yakitokea .

Comments