ALICHOFUNGUKA WOLPER KUHUSIANA NA GARI LAKE KUCHOMWA MOTO


"Kiukweli mimi kama Jacquline wolper sina ubaya na mtu yoyote, ila nimeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu.
Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni mtu mbaya sana kwangu.
Na inawezekana kabisa alipanga kuniua lakini kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafari.
Tukio lilitokoa usiku wa Tar 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani.
Nimepeleka taarifa kituo cha polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea.
Namshukuru mwenyezi mungu"
 
Wolper ambaye hivi karibuni pia amejishindia kitita cha Tsh milioni moja na zawadi  kemkem baada ya kuibuka mshindi katika shindano la ijumaa sexiet girl lililoandaliwa na gazeti la ijumaa,Akiwaacha mbali wenzake ambao ni wema sepetu na agness gelard

Comments