Kuna matatizo malimbali ya ngozi yanayoweza kuwapata watu ambapo makovu
ni mojawapo ya matatizo hayo.Makovu baadhi ya wakati hajawezi kuepukika
hasa iwapo makovu hayo yamesababishwa na magonjwa au ajali mbalimbali.
Makovu katika sehemu mbalimbali za mwili huweza kufunikwa na kufichwa
kwa urahisi iwapo hayapo katika sehemu zinazoonekena. Lakini iwapo
makovu yatakuwa usoni, mikononi au kifuani, huwa si rahisi kuyaficha na
mara nyingi huwakera wale walio na makovu. Watu wengi wangependa kujua
ni njia gani ambazo mtu anaweza kutumia ili kuondoa makovu. Ili kulijibu
swali hilo ni bora kwanza tujue kovu ni nini hasa. Kovu katika mwili
hutokea pale tishu aina ya fibrous inapojikusanya juu ya ngozi ili
kusaidia kukarabati seli na ngozi iliyoharibika. Wakati kunapotokea
jeraha, ngozi kutoa seli ziitwazo fibroblasts ambazo hutoa kitu
kiitwacho collagen na kujaza sehemu yenye jeraha. Collagen ni ngumu, iko
kama ufumwele unaopatikana katika protini ambayo hujaza eneo lote le
kovu. Collagen ipo pia katika ngozi ya kawaida lakini katika kovu huwa
nyingi na iliyojipanga katika mpangilio holela. Hii ndio sababu kovu
huwa na rangi iliyokolea na huonekana kwa urahisi. Baadhi ya makovu
huondoka kwa urahisi, baadhi huchukua miezi na hata miaka, huku makovu
mengine yakibadilika polepole rangi na muonekano wake. Kovu huenekana
kirahisi juu ya ngozi kwa sababu seli zilizotumika kuunda kovu
hutofautiana na seli za mwanzo za ngozi. Kwa mfano makovu yaliyo juu ya
ngozi hayawezi kuota vinyeleo kwa kuwa seli zake hazina matundu ya
vinyeleo. Pia makovu hayana uwezo wa kuzuia miale ya jua. Kwa bahati
mbaya ni vigumu kidogo kuweza kuondoa baadhi ya makovu moja kwa moja
katika ngozi. Ingawa kuna njia kama vile vipodozi vinavyoweza kuziba
makofu na njia nyinginezo za kitiba, lakina hata hivyo njia zote hizo
mara nyingi huwa haziwezi kuondoa baadhi ya makovu kabisa, hasa yale
makovu yaliozama katika ngozi na kuharibu kwa ngozi kwa kiasi kikubwa.
Njia za tiba zinazoweza kutumiwa kuondoa makovu ni kama vile operesheni
ya Laser (laser sugery), sindano za steroid, kubandua ngozi ya juu
(dermabrasion) na radio therapy.
Lakini hata hivyo kuna njia mbalimbali za tiba asilia ambazo zinaaminika kuweza kusaidia kuondosha makovu. Njia hizo ni kama
Lakini hata hivyo kuna njia mbalimbali za tiba asilia ambazo zinaaminika kuweza kusaidia kuondosha makovu. Njia hizo ni kama
1. Majani ya Aloe Vera. Majani haya yanapatikana kila sehemu hasa kwetu Tanzania na kwingineko Afrika. Majani hayo pia ni dawa nzuri ya kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vile kiba au kishilingi. Kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu. Baada ya muda polepole itapunguza na kuondoa makovu. Aleo Vera ni majani ambayo yanasifika hivi sasa ulimwenguni kote kwa ajili ya ngozi na yanatumiwa katika vipondozi mbalimbali. Basi zaidi ya kukuondoa makovu, yatasaidia pia kuifanya ngozi yako iwe nyororo.
2. Njia nyingine ni kutumia tango. Twanga tango na tumia mchanganyiko wake kupaka juu ya kovu. Husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.
3. Kupaka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Njia hii inaweza kurudiwa mara kwa mara hadi pale kovu litakapotoweka.
4. Kula vyakula vyenye vitamin E, ambavyo ni ni muhimu katika kusaidia ngozi kupona na kurudia katika hali yake ya kawaida. Vitamin E iko katika mayai, nyungu za aina mbalimbali kama karanga, mayai, mafuta ya nafaka na vinginevyo. Kama huwezi jitahidi utumie vidonge vya vitamin E lakini baada ya kupata ushauri wa daktari.
5. Kupaka baking soda kidogo na maji sehemu yenye kovu na kuikanda sehemu hiyo kwa dakika moja. Mara mbili kwa siku. Kisha safisha kwa maji ya vuguvugu halafu paka mafuta ya zaituni.
6. Kutumia cream zenye vitamini E nad C na upake moja kwa moja katika kovu. Husaidia ngozi kuota tena katika kovu. Unaweza kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi naye akakushauri ni cream gani utumie ili kuondoa makovu yako. Pia jitahidi kupata lishe nzuri bila kusahau matunda na mboga mboga ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi. Kunywa maji ya kutosha kwani maji pia kulainisha ngozi yako na kufanya makovu kutoka kwa urahisi.
Inafaa kujua kuwa baadhi ya makovu kama vile yaliyosababishwa na kuungua au kuchanjwa ni vigumu kuyaondoa kwa kutumia njia hizo zilizotajwa.
PIA UNAWEZA KUONDOA MAKOVU NA MABAKA KUPITIA LIMAU
Limau kulina tindikali aina ya citric ambayo inasaidia kuponya chunusi.
Vilevile tunda hilo lina Vitamin C ambayo ni muhimu katika kuifanya
ngozi iwe na afya wakati alkali inayopatikana katika limau nayo husaidia
kuua vijidudu vinavyosababisha chunusi.
Kunywa juisi ya limau kama chakula cha kwanza asubuhi kunaaminika kusadia kuboresha ngozi.
Jinsi ya kutengeneza nyumbani mchanganyiko wa limau kwa ajili ya kutibu chunusi:
• Kwa kutumia pamba paka maji ya limau katika sehemu yenye chunusi na wacha kwa usiku kucha.
• Safisha kwa maji safi asubuhi inayofuata.
• Ingawa unaweza ukahisi kuwashwa wakati unapopatumia mchanganyiko huo juu ya ngozi mara ya kwanza, lakini baadaye hali hiyo huzoeleka.
Au
1. Changanya maji ya limau ulioyakamu kutoka katika kipnde kimoja cha limao na changanya na maji ya waridi (rose water) au asali nyepesi kwa kiwango hicho hicho.
2. Paka mchanganyiko huo katika sehemu za ngozi zenye chunusi na subiri kwa muda usiopungua nusu saa mpaka saa lizima.
3. Baadye osha kwa maji.
Mchanganyiko huu unapaswa kupakwa mara mbili kwa siku, bora utumiea asubuhi na jioni.
Muhimu: kutumia mchanganyiko huu hakuna madhara na ni wa asilia, lakini iwapo chunusi zinazidi au kuna vidonda vinavyoambatana na chunusi ni bora upate uchauri wa daktari kwanza.