CHEKA UNENEPE,VUNJA MBAVU

Mama: Mwanangu hebu mpigie
simu baba yako mwambie
chakula tayari
Mtoto: Sawa mama
Mtoto: Mama simpati
Mama: Bac subir kama baada ya
dakika tano mpigie tena
inawezekana ni mambo ya
network hayo.
(baada ya 5 mins)
Mtoto: Mama mimi baba simpati
simu yenyewe anapokea
mwanamke.
Mama: Kha! Sawa mwanangu
niachie mm hili swala wewe
nenda kale.
(baada ya 30mins baba akabisha
hodi akakaribishwa na bonge la
kibao hajakaa vizur akapigwa
sufuria mara mwiko ikawa balaa
kwa kwenda mbele mme
akazidiwa)
majirani wakaja kuamulia
ugomvi,kufka mme yuko chini ya
sofa hoi bin taaban
Mama"------- zako wewe
Kunifanyia mimi hivi unaenda kwa
malaya zko kuniacha nyumbani?"
Mwanangu ebu wambie majirani
yule mwanamke alipopokea simu
alisemaje?
Mtoto: Alisema, "Samahani mteja
wa nambari uliyopiga hapatikani
kwa sasa"

kuna jamaa mmoja alikuwa nchi ya uarabuni.Alipo kuwa anataka kuvuta sigara yake akagundua kwamba hana kibiriti..Bahati nzuri mbele yake kulikuwa na mwarabu,tatizo likaja kwamba hajui kiarabu,basi ili aeleweke akamwambia yule mwarabu "give me JEHANNAM"...

Kuna jamaa alikuwa anaishi karibu
na makaburi. Basi akajigundulia njia
ya kupata usafiri bila ya kulipa...
Akawa kila akikodi bodaboda au
bajaji mida ya jioni jioni alikuwa
anaomba kuachwa makaburini.....
Katikati ya safari akawa anajipaka
poda usoni na kuweka pamba
kwenye pua zake then wakati wa
kushuka anaongea kwa kubana
pua....
"Nimefika home unanidai shilingi
ngapi?!?"
.Madereva wote wa bodaboda na
bajaji walikuwa wanatoka nduki....
Siku moja akafanya mchezo huo
kwa dereva mmoja wa bodaboda
mtoto wa TANDALE kapinda
mbaya!!! Walipofika mwisho wa
safari dereva wa bodaboda
hakutishika na mapoda wala pamba
puani....
Akakomaa anataka nauli
yake!!!!
JAMAA: "Ooooooky!!!! Twende
kwenye kaburi langu nikakupe
chako....!!!"
Dereva ya boda boda kumbe
alikuwa ameshaskia story za jamaa
so akakomaa na kumwambia...
BAJAJI: "Haina noma mtu wangu....
Twende ukanipe changu nsepe...."
maana hasira nilizonazo naweza kukulamba wewe na mapoda yako
Walipofika kaburi fulani, jamaa
akagonga msalaba....
JAMAA: "Wakulu, wakulu fungueni
nipeni alfu nane huyu jamaa
ananidai nauli......!!!!"
Ghafla mkono mrefu wenye
manyoya ukatoka kaburini ukiwa
umeshika noti ya msimbazi....
DAAAH, NDUGU ZANGU ASUBUHI
KULIKUTWA PEA MBILI TUU ZA VIATU
KANDO YA KABURI, NA KIBAJAJI
!!!!!

Binti: Baba nimepata mpenzi lakini yuko mbali sana na hapa Tanzania. Yuko Uingereza, London. Kuna website moja ya watu wanaotafuta wapenzi tulikutana humo, tukawa marafiki kwenye Facebook, tumechat kwenye Whatsapp sana, juzi kwenye Skype amepropose kunioa na sasa uhusiano wetu una miezi minne. Baba nahitaji baraka zako ili uhusiano uendelee vizuri tuoane.

Baba: Dingi akaweka gazeti chini, akakuna kipara kidogo, akavua miwani, halafu akamjibu mwanae:

Vizuri sana mwanangu. Hongera kwa kupata. Sasa fanyeni mpango muoane kabisa kupitia mtandao wa Twitter, watoto mnunue kwenye mtandao wa e-Bay na wawe wanawatembelea kupitia e-mails zenu na siku ukimchoka huyu mumeo basi umuuze kwenye mtandao wa Amazon! Kizazi cha hovyo kabisa! Mnadhani kila kitu ni mtandao! Non sense!

jamaa alinunua mbuzi, akampelekea mke wake na kumpa maelekezo kama ifuatavyo;

mke wangu huyu mbuzi akishachinjwa, nyama tutapika pilau, ngozi tutatengeneza ngoma. manyoya tutatengeneza mto wa kulalia, mapembe na mkia tutauza kwa mganga, tukishakula nyama mifupa tukaisage tutengeneze chakula cha kuku, utumbo tutapikia ndizi, kichwa tutachemsha supu.

mbuzi akamgeukia nakumwambia

"hutaki na sauti yangu ukaifanye ringtone katika simu yako?"

Jamaa alizimia palepale.




Kuna kibaka mmoja kabugi,wanasema siku za mwizi 40 basi yy ilikuwa ya 39,ilkuwa hivyi
Baada ya kuiba vituvingi kwenye nyumba moja akulidhika kakomba vitu vingi si kasahau deki kuludi akabananishwa na njemba limeshiba pandezote za mwili
JAMAA:Kumbe ndio ww unatakakuni lidisha nyuma twende huku.
Baada ya safari ndefu bila ya kuona kama atamdhulu jaama anasonga tu mara kitu cha kwanza wamekipita,
MWIZI:Mmmmh!!!!!!!
Mara kitu cha pili wanakipita
MWIZI:Mmmmmh!!!!!!!!!!!???.... ..
Mara kituo cha tatu cha polisi nacho wanakipita
MWIZI:Akanza kupiga kelele jamani mimi mwinzi jamaniiiiii,jamaniiiiiiiii mimi mwiziiiiii watu kuja kumuoji yule jamaaa alikuwa anampeleka wapi yule mwizi Mmmmh unataka nimalizie,we ushajua kilicho taka kumtokea kwa mwizi

 

wikipedia: ninajua kila kitu
google: nina kila kitu
facebook: namjua kila mtu
internet: bila mimi hamna kitu
umeme: endeleeni kuongea.....

 Mlevi mmoja aliona wananchi wenye hasira wakimpiga mwizi.

Akaingilia kati na kuwaambia "mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa kuwa atakuja kama mwizi!