Wakati asilimia kubwa ya Watanzania wakiwa hawana hili walalile (pengine kutokana na uzembe wa baadhi mamlaka au watu binafsi wenye dhamana kukwepa au kuzembea kutimiza wajibu wao kikamilifu),
mamilioni ya watu sehemu zingine duniani wanajiandaa kushuhudia
historia ya kipekee kuwahi kutokea duniani, ikiandikwa kutokea katika
moja ya miji maarufu ya nchi hii iliyoko katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Tukio hili ambalo litakuwa la kwanza na
huenda pia likawa ndio la mwisho kuwahi kutokea, linatarajiwa kujiri
Januari 27 ya mwaka huu, ambapo wanaharakati wa masuala ya kijamii
wapatao 200 toka sehemu mbalimbali za dunia, watakusanyika katika kilele
cha mlima mrefu kuliko yote barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, tayari
kabisa kwa ajili ya kupaa angani na kuuzunguka mlima huo kwa kutumia
myavuli maalum ya kurukia angani, chini ya mradi ambao umepewa jina la
Wings Of Kilimanjaro (WOK), ama kwa kiswahili waweza kuuita mradi huo
kuwa ni “Mbawa za Kilimanjaro”
Ni tukio ambalo awali liliasisiwa na
Adrian McRae, mwanaharakati wa masuala ya kijamii aliye raia wa
Australia, ambaye ameeleza kuwa, lengo la kubuni mradi huo lilikuwa ni
kuchagiza ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo chini
ya mlima huo, ambazo zimejawa na uhitaji wa mambo kibao ya kimsingi.
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!