HII NDIO RIPOTI KUHUSU MVUA KUBWA ILIYOEZUA NYUMBA ZA WATU MTWARA
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Wilman Ndile amesema kuwa nyumba 45 zimeezuliwa
mapaa ikiwemo shule ya msingi Ligula, shule ya sekondari Marwa Islamic
na kanisa la Victoria Ligula
Nyumba 113 zimebomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha katika
halmashauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani na kuacha mamia ya watu
wakiwa hawana mahali pa kukaa.Amefafanua watu waliokosa hifadhi wamehifadhiwa kwa muda kwenye madarasa
ya shule ya msingi Rahaleo wengi wao wakiwa wamepoteza vitu vyao vyote.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mvua hiyo ni Mdenganamadi, Magomeni,
Mikindani, Nandope na kiangu ambapo bwawa la Maji machafu la manispaa ya
Mtwara limejaa.
0 comments: