TULIKUWA TUNATUMWA NA DIAMOND KUMZOMEA BOB JUNIOR-MARAFIKI WA DIAMOND WAFUNGUKA
KUTOKANA NA FUJO ZILIZOTOKEA HIVI KARIBUNI KATIKA SHOW YA DIAMOND PALE MAISHA CLUB,WATU WANAODAIWA KULETA FUJO HIZO WAMENUKULIWA WAKIONGEA NA MTANDAO MMOJA WA HABARI KUWA LENGO LA KUMZOMEA DIAMOND KATIKA SHOW HIYO ILITOKANA NA KISASI BAADA YA MSANII HUYO KUVUNJA MAKUBALIANO WALIYOKUWA WAMEWEKA BAINA YAKE NA WAO.


Pia hilo kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia.
Kwa upande wa msanii Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.
0 comments: