Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa Ajali ya gari majira ya saa 2 usiku ,Maeneo ya Mjini Muheza mkoani Tanga.Katika ajali hiyo msanii Hussein Ramadhani au wengi wana mfahamu kwa jina la sharomilionea alifariki hapo hapo.Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwa marehemu sharo milionea,huku ikielezwa kuwa alikuwa njiani kurejea jijini Dar es salaam,
“leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Alisema Kamanda wa Polisi Tanga

Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!