"MOYO" NGOMA KALI TOKA KWA JAYKAH FEAT DAZLAH TOKA KENYA


LEO KATIKA INTERVIEW NAKULETEA SURA MPYA KABISA KATIKA ANGA LA MUZIKI WA BONGO FLAVA.JAMAA NI MSANII MKALI ANAYECHIPUKIA TOKA PANDE ZA KENYA.NA AMESHAFANYA KAZI KAMA TATU HIVI  AMBAZO UTAZISIKILIZA HAPA KATIKA BLOG YETU.

JINA LAKE KAMILI
 Anaitwa Jahvis karani, ana umri wa miaka kumi na nane tu!! kwa hiyo bado damu changa sana na hivyo anaweza kuwa tishio kwa waliomtangulia katika gemu.
Anasema hivi kuhusiana na elimu yake "nilisomea shule ya msingi ya frere town primary school (mombasa) hadi darasa la nane, ilikuwa mwaka wa 2008, ila sikuweza kujiunga na kidato cha kwanza sababu ya ukosefu wa fedha."
HII NGOMA INAITWA WALIMWENGU AKIWA SAMBAMBA NA BUBU BOY
Walimwengu Bub by nasmiletz

JAYKAH kama anvyojulikana kiusanii ana asili ya kilifi/keywandani nchini Kenya kama anavyosema yeye mwenyewe hapa '"Natokea kilifi/keywandani, jina langu la usanii ni JAYKAH, mie ni msanii (rapper) based in local music, i like singing about wat is going on in kenyan life & what poor people are facing out there mtaani. My focus is on > poor people (poverty) challenge they face.> mapenzi how relationships is all about 'eg, you can love some1 & the respond is negative. While you can be loved & you dont love. So ni bahati nasibu"

Kwa upande wa muziki  Jaykah amesema kuwa tayari ana ngoma kama tatu hivi ambazo ameshafanya mpaka sasa,"Nina nyimbo tatu.>1st, yaitwa walimwengu ft BUBU BOY.>2nd, yaitwa sikuhitaji tena.>3rd, yaitwa MOYO FT DAZLAH
JAYKAH Ft DAZLAH - MOYO song by nasmiletz

Kiukwel jaykah anakuja vizuri kwani nimepata nafasi ya kusikiliza track  zake na zinaelekea kufanya vema katika anga hili la burudani.siku zote wahenga wanasema nyota njema huonekana asubuhi.basi nyota ya jaykah imeshaanza kuchomoza!!!!! hebu sikiliza hizi track zake kisha usisite kuacha neno lolote la kumshauri au maoni yoyote kuhusu JAYKAH katika safari yake ya muziki 

Comments

  1. poa sana hii keep up mzeiya.usilengeze kamba hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. poa sana hii keep up mzeiya.usilengeze kamba hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. poa sana hii keep up mzeiya.usilengeze kamba hata kidogo.

    ReplyDelete
  4. the archivement became after workin hard!!! so ts ur time to reach at the top.bidii ndio kila kitu

    ReplyDelete
  5. Thanks brow... Nimekusoma vilivyo

    ReplyDelete

Post a Comment

sema nasi hapa!!