Wema Sepetu Apata Zali

      Mrembo mwenye vituko Wema Sepetu mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya ya tetesi kuwa bilionea mkubwa Dar (jina tunalo) kudaiwa kujitosa 'kumsahaurisha matatizo' binti huo mwenye mvuto
Habari kutoka kwa vyanzo vyetu zinadai kuwa bilionea huyo amempangishia Wema nyumba hiyo eneo la Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam.pedeshee huyo mwenye  hela zake amejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba anampa matunzo ya hali ya juu.
      “Mtu na hela zake ameingia kwa presha kubwa, ameahidi kumpa matunzo ya nguvu. Mbali na kumpangia nyumba, ameahidi pia kumnunulia gari la kutembelea.”
Chanzo chetu kingine kilipasha kuwa Wema kwa sasa amekata shauri la kuacha kujihusisha na mapenzi ya vijana wadogo kwa sababu wengi wao wanakuwa hawajaamua kutulia kufanya maisha.
       “Hata sisi wenyewe kama marafiki zake tumemuunga mkono na tumemshauri azingatie hilo. Unajua inauma sana kupoteza muda kuwekeza upendo wako kwa mtu ambaye hana mapenzi au mtu ambaye bado anawaza kurukaruka.
“Hayo ndiyo ambayo Wema ameyatafakari na anajutia muda wake ambao aliupoteza kwenye mapenzi yasiyo na uelekeo,” kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Wema ameamua kuanza upya kwa kila kitu ili kutibu majeraha ya moyo aliyoyapata baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
       Mama mzazi wa wema sepetu alipoulizwa alikuwa na haya ya kusema“Wema aliposema anapanga, mimi na mjomba wake tulimuweka chini atuambie uwezo wake wa kupanga nyumba, fedha amepata wapi na amejipanga vipi kuendesha maisha ya kujitegemea.
“Alitujibu kwamba anapanga nyumba mwenyewe. Tulimkatalia na kumtaka aishi nyumbani lakini alikataa kwa maelezo kuwa hawezi kuishi nyumbani miaka yote kwa sababu amekua. Tumemkubalia na mimi mama yake nimeshindwa kumbana zaidi kwa sababu amekua,” alisema Mariam.

Comments