JINA LA ALBUM LAMPA UGONJWA LINAH

MSANII TOKA KATIKA KUNDI LA THT LINAH SANGA AKA LINAH AMESEMA YUPO NJIANI KUKAMILISHA ALBUM YAKE AMBAYO ITAKUWA NA NYIMBO NANE ZA MOTO LAKINI TATIZO KUBWA AMBALO LINAMUUMIZA KICHWA NI JINA LA ALBAMU HIYO
alisema itakuwa na nyimbo nane, lakini hadi sasa bado hajaipa jina huku hajajua ni nyimbo gani ambazo zitakuwepo ndani ya kazi hiyo kutokana na ubora wa nyimbo zake zote alizokuwanazo.

Alisema kuwa mpaka sasa hajajua ni wimbo gani ambao utabeba jina la album kwani anahitaji kufikiria ndipo baade aweze kupata jina litakalofaa

“Siwezi kusema kwamba albamu yangu imekamilika, hivyo kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuweza kukamilisha na kama unavyojua katika kazi lazima uwe na mipango hivyo najalibu kuangalia baadhi ya nyimbo zangu ambazo naamini zitauza albamu ili niziweke,” alisema.

linah ni msanii ambaye amefanya vizuri sana mwaka 2011 na sasa anajipanga zaidi ili mwaka aweze kufanya vizuri tena mwaka huu 2012,
nyimbo zinazompa heshima linah mpaka leo hii ni kama vile, bora nikimbie,lonely,atatamani,chozi nk

Comments