HEMEDI KUACHA KUIGIZA?

MSANII wa muziki na filamu Nchini Tanzania Hemedi aka P.H.D ametangaza kutokujishughulisha na uigizaji kwa sasa, sababu kubwa ikiwa ni kutaka kurudi darasani. hayo aliyaongea hivi karibuni kwa waandishi wa habari kauli ambayo imeleta gumzo kwa mashabiki wake wengi waliomzoea na wanaopenda kazi zake.Pia anasema pamoja na kuwa album yake ilikamilika tangu mwaka 2010, ameamua kuiingiza sokoni mwezi wa sita mwaka huu.PHD Ambaye amewahi kutesa nangoma kama vile ninchotaka,ulisema,iyee na kadhalika pia ashashiriki filamu nyingi sana hapa bongo hali ilisababisha kujizolea mashabiki na kupata heshima kubwa sana kwa hapa TZ na Ea kwa ujumla.

Hemedi anaendelea kuweka wazi kuwa albam hiyo mara kwanza alipanga iitwe “brown colour” ..lakini kutokana na sababu ambazo hakuziweka wazi sasa imebadilishwa jina na itajulakana kwa jina la “Alcohol”.

Comments