SHILOLE AZIDI KUNG'AA

MSANII wa filamu ambaye pia anang’ara kwenye muziki kwa sasa, , ‘Shilole’ ameonekana kuanza kuziteka nyoyo za mashabiki wake kutokana na juhudi anazozifanya katika tasnia ya filamu hapa bongo.MSanii huyo hivi karibuni ameonekana kupamba sana vyombo vya habari kwa kutokana na uwezo anaounesha katika filamu mbalimbali anazoshiriki kuigiza huku pia akidaiwa kuwa na uwezo wa ajabu pia katika upande  mwingine wa kucheza na mic,
     Msanii huyo ambaye amejariwa sura na umbo lenye mvuto kwa mtu yeyote mwenye macho mawili aliingia kwenye tasnia ya bongo movie mnamo mwaka 2009 na mpaka sasa ameshashiriki filamu kama vile hazina ya marehemu,Azma’, ‘Tifu la mwaka’, ‘Mafisadi wa mapenzi’, ‘Black Wear’, ‘House boy’, ‘Pigo’, ‘Zawadi ya Birthday’ na filamu ya ke mpya inayoitwa SHILOLE IN DAR

Shilole in Dar’ ni filamu ambayo itaonesha maisha yangu sambamba na maisha yangu lakini pia itakuwa na wasanii chipukizi ambao nao wataonesha jinsi wanavyoombwa rushwa ya ngono kutoka kwa wasanii wakiume ambao ni mafisadi wa mapenzi.” alisema Shilole.



Na kwa upande wa muziki  tayari ameshatunga na kurekodi wimbo mmoja ambao utafahamika kama “Majirani Lawama”. Amesema wimbo huo ameshautengenezea video na upo katika maadhi ya Mduara, ndani ya wimbo huo kawashirikisha wasanii wenzake wa filamu ambao hakutaka kuwataja majina. 

Comments