NARUDI UPYA!!!-MR NICE

MSANII aliyewahi kutamba miaka kadhaa iliyopita na kujulikana kama mfalme wa Takeu Tanzania, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’, amesema anajipaga kurudi upya kwenye game kwani anakamilisha albamu yake ambayo anaamini itakuwa kali ingawa bado hajaipa jina.


Mr Nice ni kati ya wasanii waliopata umaarufu mkubwa miaka ya nyuma, ambapo nyimbo zake kama ‘Fagilia’ ambao ulikuwa inaimbwa “kuku kapanda baiskeli, bata kavaa raizoni” ulishika kasi na kupendwa zaidi na watoto.


alisema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kurejea kwenye game lakini mwaka huu, mipango yake imekaa vizuri na watu waliodhana amepotea kabisa wakaye tayari kumuona akiwa mpya.


Alisema wapo badhi ya watu wenye rogo mbaya ambao kila siku wamekuwa wakiomba ili asirudi tena kwenye game, lakini kutokana na uwezo wa mungu anaamini mwaka huu, utakuwa wa furaha kwa wapenzi wa muziki wa Takeu.


“Sasa namalizia albamu yangu lakini siwezi kusema nimeipa jina gani, kwani nahitaji iwe zawadi kwa mashabiki wa muziki wa TAKEU, pia nawapa salamu wale ambao hawahitaji nilejee ndani game,” aliongeza.

Comments