Ukimtaja Sinta basi utakumbuka ule uhusiano uliokuwa gumzo sana hapa Bongo mnamo miaka ya 2000 hadi 2004 wakati huo Juma Nature akitoka na mrembo huyu, lakini baadae penzi la wawili hao likaingia dosari.Hivi karibuni msanii sinta amekaririwa na chombo flani cha habari kuwa amekuwa akiota ndoto za mapenzi mara kwa mara akiwa na mpenzi wake huyo wa zamani,hali inayohisiwa kuwa kuna uwezekano wawili hao wakarudiana muda sio mrefu
msanii huyo alisema hii ni wiki ya tatu tangu alipoanza kuota ndoto hizo ambazo zote humuonyesha vitu vyote walivyokuwa wanafanya walipokuwa wapenzi.
Alisema mara ya mwisho aliota wakiwa katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Coco beach, lakini hadi hivi sasa hajui nini cha kufanya kwani ndoto hizo zinamfanya ahisi bado anamapenzi mazito kwa msanii huyo.
Lakini kubwa zaidi msanii huyo amedai kuwa hiyo imetokana baaada ya wazo la kufanya nae filamu yake inayokwenda kwa jina la 'sitaki demu' ambayo pia sinta amedai ndani ya filamu hiyo anategemea kufanya na staa wa vichekesho nchini marekani "mr bean"
mwenyewe alithibitisha kwa sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na msanii huyo kutoka kule Marekani na muda wowote atatua hapa nchini kufanya kazi hiyo
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!