Wasanii wa Mbinga wamlilia mbunge John Komba


MH.JOHN KOMBA,MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI
Wasanii wanaofanya aina mbalimbali za muziki kutoka mbinga mkoani Ruvuma wametoa kilio chao wanachokielekeza kwa Mh mbunge wa jimbo la magharibi John komba.wakimlilia kwamba awasaidie kwa namna moja au nyingine ili nao waweze kufika mbali kimuziki kwa kuwa licha ya yeye kuwa ni mbunge pia ni mwanamuziki wa siku nyingi na anaweza akafanya kitu ili kuinua muziki wa mbinga na ruvuma pia.

     Moja kati ya vitu vilivyotajwa na wasanii hao kuwa vinaweza kuinua muziki wa mbinga ni pamoja na kituo cha redio japo kimoja ambacho kitakuwa kinarusha matangazo yake kutoka mbinga na kuenenea wilaya zingine na hata nje ya mkoa pia.

MMOJA WA WASANII KUTOKA WILAYANI MBINGA,JERRY ONE
    Pia wasanii hao wamemuomba mh komba kuwasaidia kwa kuwadhamini na kuwapromote kitaifa zaidi ikiwepo kuwasaidia kufikisha kazi zao katika vituo mbalimbali vya redio na television vya kitaifa ili waweze kufahamika na kupata mialiko mbalimbali.

    Wasanii hao wamesema hao katika moja ya vikao vyao kilichofanyika hivi karibuni katika studio ya muziki peke ya wilaya hiyo ya mbinga Ps records ikiwa chini ya Producer Frank ngongi.

Comments