SINA MPINZANI BONGO-DIAMOND



MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya bongo, Diamond, amesema kuwa anafikiria kuimba nyimbo za taarabu baada ya kukosa mpinzani kwenye bongo fleva.

Aidha alisema kuwa katika muziki wake hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango alichokuwa nacho kwani katika kuthibitisha hilo ndani ya nyimbo zake hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha.

Aliongeza kuwa kikubwa kinachomsukuma kufanya kila aina ya muziki ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho kwani hakuna kitu anachoweza kushindwa kutokana na uwezo aliyokuwa nao.

Msanii huyo aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.

“Naweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watastuka sana,” alisema.

Hata hivyo alipoulizwa kama anatshirikiana na wasanii wakongwe wa nyimbo hizo za mipasho, alisema kuwa kwanza atasimama mwenyewe lakini baada muda ataweza kuwashikisha vichwa kama Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na wengi kibao.

Comments