Hukumu ya Kajala ni jumatatu hii

Msanii wa filamu kajala na mumewe wanategemea kuapanda mahakamani leo hii ili kusikiliza hukumu ya kesi yao inayowakabili ya kughushi na utapeli

Wakili Swai, alidai kuwa, kosa la kwanza ni kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo la kula njama la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni kwamba, Aprili 14 mwaka 2010 walihamisha isivyo halali, umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Alidai shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha, ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14 mwaka 2010, huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
kesi hiyo ilisikilizwa mara ya mwisho wiki iliyopita ilihairishwa baada ya mshitakiwa wa pili kutoonekana mahakkamani.hivyo kuhairishwa mpaka jumatatu ya tarehe 20 mwezi huu ambayo ni baadaye leo hii

Comments