ROSE NDAUKA NA KAMPUNI YAKE

Muigizaji mashuhuri  wa filamu hapa nchini Rose Ndauka amezungumzia mafanikio yake kwa kusema kuwa yanatokana na mashabiki kumkubali.

Alisema asingeweza kufika, alipo kama mashabiki wasingetambua uwezo wake na kununua kazi zake.hali iliyopelekea kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayoitwa Ndauka entertainment.


"unajua siku zote huwezi kuwa chochote bila mashabiki,hivyo wao wakikubali kazi zako ndipo na wewe unapata mafanikio.hivyo siku zote mimi naheshimu sana mashabiki wangu na pia najitahidi kuonesha uhalisia wa kile ambacho naigiza ili kuwavutia zaidi'' alisema Rose.
Hivi karibuni ndauka alitangaza kutafuta wasanii chipukizi ambao watakuwa katika kampuni yake na kufanya nao kazi.vijana wengi walijitokeza na usahili ukaanza mara moja ambapo  vijana kadhaa walichagulliwa na sasa wapo kambini
Alisema kampuni yake kwa sasa itakuwa ikijihusisha kwenye ukuzaji wa vipaji vya wasanii tena ambao ni wapya, kutoka popote lakini ni ndani ya Tanzania.

wema sepetu nae ni mmoja kati ya wasanii wa filamu wanaomiliki kampuni zao wenyewe


Kwa sasa wameanza na mkoa Dar lakini kwa siku za baadae watafikiria waende nje ya Dar kwa ajili ya kuwachagua wasanii chipukizi ili waweze kuonyesha vipaji vyao ambavyo kuna hatari ya kupotea kwa kukosa mtu wa kuwawezesha ili waigize kwenye filamu zinazoonekana kwa kushirikisha nyota.








Hadi sasa mwanadada huyo amefanikiwa kwenye kuongoza filamu kadhaa ikiwemo pamoja na filamu aliyoiandaa mwenyewe ya Bad Girl.
Mbali na hiyo kuna filamu ambayo ipo jikoni muda si mrefu itakuwa sokoni kwa ajili ya mauzo

Comments