WEMA ASIMULIA ALIVYOKUTANA NA DIAMONDI SIKU YA KWANZA


WEMA ALIPOKUTANA NA DIAMOND SIKU YA KWANZA

Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu). 
Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu. Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda.
 So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta. Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia. Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. 

Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikumuuliza anakataa. Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. 

Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja.

0 comments: