JINSI WEMA SEPETU ALIVYOKUTANA NA KANUMBA SIKU YA KWANZA


Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada yangu. Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana protective kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya pale nyumbani kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different furnitures, so tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la Mwanamboka kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda pale wakati tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao nini ,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, tumepark gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya tukasalimiana akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na mimi napenda unavyoigiza’ nini na nini.
Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani
kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’. Nikamwambia
siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle Hashimu wataniua
wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila kuwaconsult so
akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati ananiambia tuachie
nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja umemuona Wema?’
Aliniringia sana. ‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia
poa,’Kaka basi chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza
tukamtumia kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani.
Basi nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza,
‘Hee Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao. Basi, so baada ya
hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep nikamsave, basi mimi
nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba inanipigia ambayo nimeisave
vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’ akaniambia ‘vipi, safi
Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’ ‘haya basi sawa basi
baadae’ nikamwambia ‘poa’. Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext
‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi uko wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia
ya kutextiana kila siku tunandelea for one weak tunatext mara yeye
ataniuliza umekula nini, mara sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu
unajua kwamba mwanaume akiwa ana interest na wewe.
Kidogo tukaanza
kuulizana una boyfriend una girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia
mimi ‘nipo kambini Lamada’ akanielekeza nikafika. Basi nimefika siku
hiyo tumekaa pale garden akaniambia ananipenda na nini, hivyo. Kipindi
hicho nilikuwa sina boyfriend nilikuwa very very single, so
nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na boyfriend wangu sijui nini’
akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie basi’ Nakumbuka tulivyokuwa
tunaondoka ndo tukakiss, it was our first kiss. Basi nikaondoka,
akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia siwezi akaniambia please,
please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia ‘sawa’ basi nikarudi then
akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi yakaanza. Basi kwenye
mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact movies na wewe’
nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi unaweza kuact
hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia ‘unaweza
kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’ akaniambia ‘basi
kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu ukimenya si unalia,
basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ . Akaniambia niende kuonana na
bosi wake. Nilivyofika tu ofisini nikaonana na Mtitu Game. Akanipa
script akaniambia nikasome kama story akaniambia ‘wakati unasoma uwe
unasoma sana concentrate kwenye Dina.
Basi vile tukiwa tukikutana
tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa basi wewe you are ready to
shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, hauwezi amini, I just felt
yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa wengine wanaona it’s hard
unajua. Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back
to school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka
ya International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu
ya Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona
kwamba kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo
soon naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’ Nimerudi
kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White Maria yaani
tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa nimeshajikuta
katika movie, so that why I keep saying kwamba without him nisingejua.
haya ameyasema yeye mwenyewe alipofanya mahojiano na mtandao flan hapa nchini
0 comments:






