CHEKA UNENENEPE.NDUGU YANGU

 Jamaa alikuwa ana tabia ya kukojoa kitandani baadhi ya siku.
Akafikia kuoa. Katika ya siku za mwanzo baada ya harusi, siku moja kama kawaida yake alijikojolea.
Akapiga kelele “Mungu wangu eee”.
Mke wake akashtuka, akamuuliza: Vipi mume wangu?
Mume: Hivi mke wangu ungeota unataka kuliwa na mamba, chuwi na simba kwa wakati mmoja ungefanyaje?
Mke: Ningezimia kabisa.
Mume: Basi mwenzio sijazimia nimejikojolea.


Hivi tuchukulie wewe ni mwalimu unafundisha kidato cha kwanza somo la kiswahili, siku moja ukiwa katika mazungumzo ya kawaida mbele ya darasa ukatamka “usilolijua ni kama usiku wagiza”, baada ya kumaliza ulichokuwa unazungumza mwanafunzi akanyoosha mkono kuzungumza na ukamruhusu, akasema “mwalimu kutokana na maendeleo ya sayansi UKITUFUNDISHA kuwa usichokijua ni kama usiku wa giza utakuwa unatufanya tusiwe wadadisi na kufunguka kielimu na kufanya hivyo si sahihi, ila sahihi ni kusema kuwa USILOLIJUA KAULIZE GOOGLE.

Wewe kama mwalimu utakubali kubadilika na kufuata mafundisho ya mwanafunzi wako na utatoa jibu gani?

Mlevi mmoja alikuwa anakula ugali na samaki, mkewe akamwambia “Mume wangu angalia miba isije ikakuchoma”, Mlevi akajibu “Usijali mke wangu nimevaa viatu”
,......................................................................
Kichekesho cha msichana wa kazi za nyumbani na mama mwenye nyumba juu ya vijiti vya kusafishia meno.

jamani nyie watoto wa nyumba hii, vijiti vya meno nimeleta juzi tu leo vyote vimeisha, mnazipeleka wapi?”

Ndipo hoousgirl akadakia na kusema “mama mimi simo humo maana kila nikitumia nikimaliza tu navirudishiaga humo humo”

Kwa wale mnaotumia sana usafiri wa umma au daladala utakuwa umekumbana na mojawapo ya ya vituko vya makonda na abiria wa daladala kama ifuatavyo

Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
Konda; Yesu bado hajatoa albam.
Matozi; humu ndani joto
Konda; kapande friji
Abiria; kuna siti?

Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?

Sistaduu: Konda unanibana
Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!
Mama: sikai siti za mwisho
Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?
Abiria : we konda  vipi kuwa  kama umeenda  shule
Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule
Kama una mengine tafadhali ututumie na tutakuwekea kiunganishi cha blogu au web yako hapa bure