KUWA MAKINI..HIZI NDIO AINA MBALIMBALI ZA JINSI WATU WANAVYOIBIWA,KUPORWA NA KUTAPELIWA JIJINI DAR ES SALAAAM

NIMEJARIBU KUPITIA MAONI YA WATU MBALI MBALI WAKISIMULIA JINSI WALIVYOWAHI KULIZWA NA WEZI,MATAPELI HAPA BONGO DAR ES SALAAAM...SOMA MWENYEWE MIKASA MBALIMBALI ILI USIJE UKALIZWA NA WEWE.....



Wezi wa usiku hasa mitaa ya sinza madukani hadi kumekucha wameibuka na staili mpya ya wizi ambayo wanaiita chipsi mayai. staili hii jamaa huchukua jiwe na kulibeba kwenye mfuko mweusi kama chipsi vile ukipishana naye tu anakutandika nalo kisogoni hadi network zinakata na baada ya hapo anakusaula kila kitu.

Jamani kuweni makini siku hizi hasa mitaa ya Posta na Kariakoo kumeibuka mtindo wa aina yake ya uporaji kwa abiria kwenye Taxi. Kinachofanyika hasa mida ya jioni kuna Taxi huwa zinasanya abiria watano kwa elfu 2 toka Posta na Kariakoo kumbe ndani ya wale abiria wanne pamoja na dereva lao moja wewe ukiongezeka kutimiza idadi ya watano gari inasepa lakini wanakupeleka chobingo na kukupora Simu, pochi, saa na hata viatu n.k
Kuweni makini na Taxi 'bubu' hizo za mujini

Kuna aina mpya ya utapeli ambayo imeingia jijini Dar. Kuna wajanja fulani ambao wanatumia fursa ya kwamba kila anayepigiwa kelele za Mwizi Mwizi Mwizi hadharani atasulubiwa bila ya kuhojiwa, wamezua mtindo wa kuwaomba watu simu zao, wajifanye wanabip, kisha wanapigiwa, wanawaomba waliowapigia wawatajie namba ya simu waliyoitumia - kwa kuwa ni washirika wenzao katika dili - ili baadaye waje kudai kuibiwa simu.
       Katika purukushani ya kumtafuta Mwizi huyo wa simu, ambaye si mwizi, ila yule ambaye anayedai kuibiwa ndiye mwizi halisi, inatajwa namba ya simu inayodaiwa kuibiwa. Inapolia, inaita kwa mtu ambaye si mhusika, hapo hapo anaanza kusulubiwa bila kuhojiwa.
          Hii tabia mbaya yetu sisi kuamua kuchukua sheria mkononi pasi na kuhoji ukweli wa tuhuma sasa inawafikia pabaya raia wema. Kaeni chonjo, msije kuitwa wezi. Ushauri: Mtu usiyemfahamu akikuomba simu yako akabip kataa kata kata, mwambie simu yako haibip hata siku moja, anakushusha hadhi! Akisema si wewe unayebip, unamwambia hata kama si wewe! Akileta za kuleta unamkata kibano cha nguvu na kumpigia kelele za Mwizi Mwizi, wamsulubu yeye!

Jamani kuna wimbi la matapeli wa fedha za kigeni nje ya maduka ya kubadilishia hizo fedha pale Posta karibu na SH Amon au Akari monoument. Juzi ndugu yangu wa karibu sana alienda kubadilisha US $ 4000 akakutana na jamaa wakidae eti wana rate nzuri zaidi ya zile za kwenye maduka ya kubadilishia fedha akakubaliana naio watambadilishia kwa TZS 1520 kila dola moja akaingiwa na tamaa wakambadilishia na akahesabu fedha zote zikatimia kwa mijibu wa mahesabu ya dola 4000. Kufika nyumbani lahaula! akaambulia noti 5 ta elfu kumi na mia tano kibao amabazo jumla yake ni TZS 165,000 kati ya TZS 6,080,000 alizozihesabu yeye mwenyewe kwa umakini na uhakika. Sasa cha ajabu ni vipi hizo milioni kadhaa zimegeuka kuwa vijisent vichache sijui wanatumia mazingaombwe ama vipi?? Kwa hiyo jamani tuwe makini ukienda popote kubadili fedha za kigeni hakikisha unabadili kwenye Beaureu de change na si vinginevyo kwani nasikia hawa matapeli kumbe wako siku nyingi na polisi wanawafahamu lakini ndio hivyo tena hii ndio Bongoland...

Kuna bwana mmoja miraba minne pandikizi la mtu mwenye lafundi ya kaskazini anazunguka katika mabaa usiku na kutafuta watu wa kuwatapeli.
Ukiwa na marafiki unapata kinywaji huyu bwana anakufuata na kuanza kukuchangamkia kama vile anakujua, baadae atakuuliza wapi anaweza kupata mwanamke.
Baada ya muda atakuonyesha gari yake ni corolla limited nyeupe na kukuambia ndio anaingia kutoka arusha na amekuja dar kufuata mzigo kariakoo, ukiangalia gari yake kweli utaiona imechafuka vumbi/matope. (si kweli kwani wanaipka vumbi/matope).
Baada ya muda atakuuliza wapi anaweza kupata huduma ya intaneti ili aweze kuhamisha pesa zake kwako halafu wewe utoe kiasi cha pesa alichohamisha mtumie kunywa na kutafuta mabibi.
Ukijisahau ukamkubalia na kuingia kwenye gari yake basi unaporwa kila ulichonacho, huyu jamaa mawindo yake ni kinadada na wengine ambao wamelewa....kuweni macho, anazunguka maeneo ya ambiance corner bar na kwingineko jijini dar es salaam.

mimi niko amerika, najenga nyumba yangu hapo dar, fundi anayejenga nyumba amenipigia simu kuwa watu hao wa TANZANIA JAPAN ORPHON PROJECT WA SIMU NUMBER 0783-927-196 MR SABAI wana hitaji nyumba ya kupanga kwa miaka 2 kwa dola 800 jumla watatoa dola 19,200.00 kwa ajili wafanyakazi wao, wakasema watajenga fence ya umeme kuzunguka nyumba, kuchimba kisima cha maji, watamalizia kuweka umeme kama offer . Lakini baada ya kupata habari hiyo nikapiga simu kwenye ubalozi wa japan hapa USA wakasema hakuna shirika la namna hiyo na wakanitajia majina kama hayo uliyoolezesha kuwa ndiyo wamiliki wa shirika hilo haramu.OK WANAIBAJE? watakupeleka kwa wakili wao ambaye pia ni taperi mwenzao, unasaini mikataba mingi usiyoilewa na kwa vile mawazo yako yote yako kwenye lundo la pesa ya miaka miwili unasaini tu, lakini akili yao ni kukusainisha mkataba kwamba unawauzia nyumba kwao kwa bei hiyo ya kupanga kwa miaka miwili, sasa kwa vile wewe hujui baada ya miaka miwili ya mkataba wa kupanga kuisha ukiwambia ku-renewal mkataba watakucheka kwamba wewe uliwauzia nyumba, na ni kweli umesaini tena kwa wakali!!! kuweni macho sana.

Jamani kuweni macho na wezi hawa,akina dada/mama=wanawake kadhaa hapa jijini wamekwapuliwa handbags/pochi wanazoninginiza mabegani na wezi hawa.yaani wao wanatembea na bajaji ,pikipiki, tax,magari madogo ya abiria ,wanaendesha mwendo wa taratibu usawa wa mama /dada mtembea kwa miguu akiwa na pochi/handbag lake begani au mkononi.wakishamfikia tu wanalikwapua /wanakupua kwa nguvu na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.kwa kuwa mlengwa anakuwa kama ameshitukizwa na pia kushtuka kwa tukio, bado anakuwa haamini kilichotokea na hivyo huduwaa.huku mkupuaji akimwacha kwa mbali na waliokaribu kuanza kuelewa kilichotokea.akina mama /dada chukueni tahadhari na jaribuni kuripoti matukio haya polisi.pia ukiweza chukua/andika namba za chombo husika katika tukio.je wanajamii hili mnalionaje?