UMEKWAZIKA LEO?? NA UNAHITAJI KUFURAHI NA KUVUNJIKA MBAVU?? SOMA HAPA


Jamaa alionekana kapona hivyo atolewe kwenye hospitali ya machizi arudishwe kwao. Asubuhi mmoja akachukuliwa na ambulance mpaka jirani na kwake, akaulizwa unapafahamu hapa? Akajibu ' Ndio nyumba yangu ileee". Ghafla mlango wa nyumba ile ukafunguka wakatoka watoto wawili wamevaa yunifom,'Hee na watoto wangu walee wanaenda shule'. Mara akatoka mwanamke, jamaa akafurahi,' Mke wangu yule, mke wangu jamani'. Madaktari walianza kumfungulia atoke kwenye gari ghafla mwanaume akatoka kwenye ile nyumba, jamaa akaangalia kwa makini kisha akaruka kwa furaha,' Mimi yulee naenda kazini, unaona nilivyopendeza na suti ile nilinunua Mariedo'. haraka sana akarudishwa hospitalini.
.......................................................................
 mume-mke wangu nambie kitu gani unachotaka nikupe ili ujue nakupenda! mke- TALAKA!
.................................................................
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;

MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu, huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya kulevya.

MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia kwa kujenga eneo la choo we toa tu
......................................................................
..........................................................................
Jamaa katika uhuni wake akakumbana na ugonjwa wa ajabu akavimba sehemu za siri, akaenda kwa daktari ambaye akamuangalia kwa makini;

DAKTARI: Umetembelea nchi ya Malawi karibuni?

JAMAA: Ndio dokta

DAKTARI: Na ukalala na mtu huko?

JAMAA: Ndio dokta
DAKTARI: Basi umepata ugonjwa unaitwa NYASALIASIS

JAMAA: Duh, dokta nisaidie nipone

DAKTARI: Ni ngumu kidogo maana wote waliougua ugonjwa huu wanakufa , lakini sijui labda tufanye operesheni.

JAMAA: Hakuna njia nyingine dokta, unajua hapo mahala pabaya, sasa kufanya operesheni hapo dah

DAKTARI: Jaribu sehemu nyingine lakini kwa kweli mi nadhani operesheni labda ingesaidia. Jamaa akatoka akaenda kwa mganga wa kienyeji


JAMAA: Aise nimepimwa nimekutwa na NYASALIASIS, sasa dokta anasema watanifanyia operesheni....Mganga akamwambia avue nguo, nae akamcheki, akaanza kucheka sana

JAMAA: Vipi mbona unanicheka?

MGANGA: Unajua madaktari wenu bwana hili tatizo dogo wanazunguka eti wanataka kukufanyia operesheni, yanini operesheni?

JAMAA: Utaweza kuniponesha?

MGANGA: Hapana, ila hakuna haja ya operesheni, mbona hii baada ya wiki itakatika yenyewe.
 

....................................................

Jamaa kagongwa na baiskeli, mwendesha baiskeli akaanza kumnyanyua jamaa;

MWENDESHA BAISKELI: Aise una bahati sana

JAMAA: Umenigonga na baiskeli halafu unanambia nina bahati

MWENDESHA BAISKELI: Ni kweli maana kwa kawaida huwa naendesha daladala