Tangu kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda Osama
bin Laden kumekuwa na fununu nyingi zinazoeleeza mazingira ya kifo
chake pamoja na ujumla wa maisha yake wakati akiwa mafichoni
Tangu kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda
Osama bin Laden kumekuwa na fununu nyingi zinazoeleeza mazingira ya kifo
chake pamoja na ujumla wa maisha yake wakati akiwa mafichoni. Katika
mfulilizo wa makala haya, Mwandishi George Njogopa amepitia simulizi za
askari aliyemuua kiongozi huyo kama alivyozungumza na mwandishi mmoja wa
habari nchini Marekani.
Akiwa mtu mwenye tabasamu na ucheshi wa
mbali, askari (jina linahifadhiwa) anatoa maelekezo kwa mwandishi wa
habari aliyetaka kujua historia ya maisha yake jeshini. Ndani ya mgahawa
uliofurika watu waliochangamka kwa vinywaji, askari mwanamaji anaanza
kueleza namna alivyojiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani hadi kufikia
nafasi ya kuwa mlenga shahaba mkuu.
Anasema anakumbuka kile
kilichomsukuma kuchukua uamuzi wa kujiunga na jeshi ni kama sehemu ya
hasira iliyomkumba baada ya kuachwa na mpenzi wake al iyedumu naye kwa
kipindi kirefu.
“Unajua tukio la kuachwa na mpenzi wangu lilinivunja moyo sana… na ndiyo nikachukua uamuzi kwenda jeshini.
Anasema
kuwa siku yake ya kwanza alipokwenda kuomba kazi anakumbuka alimwambia
ofisa mmoja wa jeshi kuwa alikuja hapo kuomba kazi ya kulenga shahaba
(sniper).
“Pale nilimkuta askari mfukuzi, mkufunzi akaniuliza
unataka nini… nikamwambia nataka kuwa mlenga shahaha, lakini yeye
akaniambia kuwa tayari walikuwa na walenga shabaha.
Hata hivyo
alifaulu kuandikishwa na baadaye kupelekwa kwenye mafunzo
yaliyimwongezea ujuzi wa kazi na hatimaye kuungana na vikosi vya
wanajeshi wa maji vilivyosafiri sehemu mbalimbali duniani. Kama ilivyo
kwa askari wengi wanamaji, askari huyu alishiriki kwenye operesheni
mbalimbali za kijeshi ikiwemo zile zilizohusu katika nchi za Afghanistan
na Iraq.
Anasema operesheni yake kubwa ya kijeshi ilikuwa nchini
Afghanistan ambako vikosi vya Marekani vilivamia katika eneo hilo katika
kile kilichoelezwa na kukabiliana na utawala wa Taliban ambao ulitajwa
kuwa na ushirikiano wa karibu na Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda.
“Uzoefu
mkubwa wa kijeshi niliupata wakati nikiwa Afghanistan ambako nakumbuka
nilishiriki kikamilifu kukabiliana na wanamgambo wa Taliban. Tulipofaulu
kuwafurusha wanamgambo hao tuliendelea kubakia nchini huko kuimarisha
hali ya usalama na kusaidiana na wananchi wa eneo lile kurejesha hali ya
usalama.
“Kichwa changu kilikuwa tayari kimeshazoea mizinga na
makombora, maana wakati mwingine umekaa sehemu ghafla unasikia kombora
linavurumishwa mbele yako… Ghala nyuma unasikia mlio wa bunduki.. Kusema
kweli nilijifunza mengi wakati nikiwa Afganistan.
Wakati huo
Marekani ilianzisha operesheni za kukabiliana na Kundi la Al-Qaeda
ambalo lililodaiwa kutekeleza tukio la kigaida katika majengo yake mjini
New York na Washington.
Shabaha ya Marekani ilikuwa kukabiliana
na kiongozi wa kundi hilo, Osama bin Laden ambaye wakati huo ilisemekana
amejichimbia mafichoni katika Milima ya Afghanistan.
Marekani
haikuishia kuingia kijeshi nchini Afghanistan pia iliivamia Iraq na
hatimaye kuuangusha utawala wa Saadam Husen aliyekuwa akiongoza Chama
cha Baath ambacho kilikuwa na uhusiano pia na baadhi ya makundi ya
kigaidi.
Anakumbuka kuwa jinsi alivyorejea nyumbani Marekani na
kisha kuungana na wanamaji wenzio ambao waliunda kikundi cha wataalamu
wachache walikuwa na shabaha ya kuleta mageuzi ya utendaji ndani ya
vikosi vya wanamaji hasa kwa kutumia uzoefu waliopata wakati wakiwa
kwenye operesheni za kijeshi katika nchi za kigeni.
“Unajua
ukishajiingiza kwenye mambo haya ya kulenga shabaha hujali tena lolote,
wewe unachoona ni kwamba umeletwa duniani kwa kazi maalumu na hiyo kazi
lazima uitekeleze kwa wakati uliopangwa,” anasema askari huyo
akimwelezea mwandishi mmoja wa habari namna alivyoshiriki kwenye kikosi
maalumu kilichoshiriki kwenye operesheni ya iliyofanikisha kuuawa kwa
kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda, Osama bin Laden.
Kwa masharti ya
kutotajwa jina wala kuonyeshwa picha yake, askari huyo anasema kuwa,
“Tulipomaliza kazi nchini Afghanistan tulirudi nyumbani na kuendelea na
mazoezi yetu ya kuogelea katika Ufukwe wa Miami. Tukiwa kule ghafla
tukapata taarifa baadhi yetu tulihitajika kwenda Virginia kwa ajili ya
kazi maalumu.
“Kusema kweli hatukujua nini tunachokwenda kukifanya
maana tulielezwa kuwa kuna kazi ya dharura. Wengi wetu tukabaki
tunahisi labda tunataka kupelekwa Libya, wengine wakasema labda tutaenda
Japan kukabiliana na athari za kimazingira baada ya tetemeko kubwa la
ardhi kulikumba taifa hilo.
Katika siku ya kwanza tulivyopata
taarifa, kusema kweli walitudanganya. Tulizungushwa maeneo mbalimbali na
kila mara maofisa wetu walikuwa wakitupa maelezo ya kutia matumaini
wakisema kuwa tusiwe na wasiwasi tutaarifiwa punde kwani kulikuwa hakuna
jambo lolote la kutisha.”
Anasema kuwa baada ya kukaa kwa siku
kadhaa walipelekwa moja kwa moja hadi yaliko makao makuu ya upelelezi
CIA, ambako walipokewa na maofisa wa ngazi juu aliyewagawanya kwenye
vitengo bila kuwapa maelekezo yoyote.
“Wakati tunakwenda
tuliambiwa tungekutana na Waziri wa Ulinzi, maofisa wa ngazi za juu wa
jeshi pamoja na wataalamu wengine wa kijeshi. Tulipata hisia jambo
tulioloitiwa huko huenda likawa kubwa. Tulipofika pale tulikusanywa
kwenye chumba kimoja na baada ya muda alitokeza mwanamke mmoja ambaye
kwa sura alionekana kuwa mtu jasiri na mwenye kuelewa kile
anachokizungumza.
“Tuliona tumeletewa televisheni..vifaa vya
kivita na pembeni kulikuwa na ramani kubwa ambayo hata hivyo ilifunikiwa
na kitambaa . Hatukujua kile kilichokuwa kinaendelea. Yule mwanamke
aliposimama ndipo pumzi ikatushuka,” Anaelezea kuwa walipatiwa maelekezo
kuhusiana na sehemu ambayo inasadikika Kiongozi wa Al-Qaeda, Osama bin
Laden ndiyo ilikuwa makazi yake.
“Yule askari wa kike akiwa katika
hali ya kujiamini, alituonyesha ramani na kutufafanulia shabaha ya
kuitwa kwenye chumba kile. Nilishtuka lakini kadiri nilivyomtazama yule
askari niliamini kile alichokuwa akikisema. Tulionyeshwa nyumba moja
ambayo iko pekee yake katika eneo la Abbottabad.
Baada ya hapo
tukaingia kwenye mazoezi makali tukijifunza namna ya kuingia kwenye
nyumba ile na namna tukavyoweza kumudu purukushani zozote zinazoweza
kujitokeza.
Mafunzo yetu yalidumu kwa muda wa wiki kadhaa na kisha tulipangiwa siku ya kuondoka kuelekea Pakistan.
Anasema
kuwa msafara wa kuelekea Pakistan alianzia nchini Ujerumani walikoweka
kituo na kisha kuruka moja kwa moja hadi nchini Pakistan kupitia eneo la
Jalalabad.
“Unajua wakati tunakatiza anga ya Pakistan niliingiwa
na hofu sana pengine vikosi vya pale vingeilenga ndege zetu na
kuzitungua maana kulikuwa hakuna taarifa zozote kwa Serikali ya Pakistan
kuwa Majeshi ya Marekani yalikuwa yakiingia nchini humo.
Tulipita
eneo lile na hatimaye kufika Abbottabad. Tulikuwa tumejipanga vya
kutosha. Msafara wetu ulikuwa na helikopta, ndege za kivita pamoja na
vifaru kukabili hali yoyote korofi ambayo ingejitokeza.
Nilishangaa
kuona kile nilichoonyeshwa kwenye picha za satelaiti wakati nikiwa
kwenye mazoezi Marekani ndicho nilichokishudia pale.
Tulishuka
kwenye helikopta haraka na kisha kuizingira nyumba mara moja. Kuna
wengine walitanda juu ya paa, wengine madirishani na wengi walikuwa
angani kwenye helikopta.
Tulipofika mlangoni tulikuta tundu la
risasi, tukashtuka kidogo, nikamwambia mwezangu acha woga hebu twende,
nikasukuma mlango hadi ndani.
Wakati kabla hatujaingia ndani
tulisikia sauti ikiita bla, blab la,,, kumbe ilikuwa sauti ya mmoja wa
walinzi wa Osama ambaye alikuwa amevalia fulana nyeupe na pajama nyeupe
pia.
Tulimdhibiti na kupanda hadi ghorofa ya pili ambako tuliwakuta kina mama wakiwa wanahangaika na kupiga kelele.
Hatukutaka kuwadhuru tuliwaweka chini ya ulinzi, nami nikaendelea kupanda juu hadi ghorofa ya tatu.
“Nilipofika
chumba cha juu nilimwona mtu mmoja mrefu kupita wote, ndevu zake
alikuwa ameonyoa kiasi. Alikuwa ameweka mikono yake begani kwa mwanamke
mmoja ambaye baadaye nilikuja kugundua alikuwa mkewe Jamal.
Nadhani
alikuwa anafanya vile kama njia mojawapo wa kujikinga. Alikuwa amevalia
kofia na kuendelea kuzunguka huku na kule na yule mwanamke.
Nakumbuka alikuwa mwembamba. Pembeni yake kulikuwa na silaha aina ya AK 47, ambayo baadaye aliishika mkononi.
Binafsi
sikutaka kupoteza muda, nilinyanyua bunduki yangu na kumiminia risasi
mbili usoni na kisha nikamshudia namna alivyoanguka chini na kukata
roho. Sikujali kama amekufa ala nilimmiminia risasi nyingine moja.